Mwigizaji wa kike wa filamu Ligth butterfly Mushi ‘Light’ amefunguka kwa kusema kuwa hapendi kuigiza Komedi kwa sababu ni udhalilishaji hasa kwa wanawake, anasema kuwa aliwahi kuchaguliwa kucheza Komedi ya Inye lakini baadae aligundua kilichofanya achaguliwe ni maumbile yake.
“Tunaigiza filamu hakuna udhalilishaji lakini kuna Komedi tuliwahi kucheza ilikuwa inataka wasanii wa kike wawe na maumbile makubwa yaani makalio, kuchesha makalio sasa huo si uchekeshaji ni udhalilishaji, hicho ndio kilinifanya nichukie Komedi,”anasema Light.
Light anasema kuwa waandaaji wasiangalie tu maslahi yao tu pia waangalie waigizaji nao maisha yao baadae wakiwa na familia zao na wakiangalia filamu zao za Komedi zilizotolewa siku za nyuma watakuwa katika hali gani, hali ambayo inamfanya asipende kuigiza Komedi
Sipendi Comedi za Kibongo Kwa Asilimia Kubwa zinazalilisha Wanawake
2
February 19, 2015
Tags
Sizitaki mbichi hizi"alisemaga Sungura
ReplyDeleteKWELI KABISA NI UDHALILISHAJI HAPO NAKUUNGA MKONO!!!!
ReplyDelete