Vurugu Ilula Mkoani Iringa, Mwananchi afariki, Kituo cha Polisi chachomwa moto!

Wananchi wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa,  wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo  kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake wakati anakimbia alichotwa mtama na Polisi na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo .
 
Mama huyo alikuwa anawakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita,  hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
 
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.


Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAHENGA WALISEMA"USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA"

    ReplyDelete
  2. WAHENGA WALISEMA"USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA"

    ReplyDelete
  3. Askari wetu badilikeni, badala ya kuwa watetezi wa raia mumekuwa kila siku mnajenga uhasama na raia, sijui mtawezaje kuzuia uhalifu kwa hali hii.

    ReplyDelete
  4. HIVI WEWE ASKARI ULIYEMKATA MTAMA MAMA HUYO UNAJIKISIAJE??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad