Udaku Special Blog: Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayemkamata kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha Sajuki.
“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
GPL
Wastara Awacharukia Wanao Mtukana Mumewe Mitandaoni...
4
February 09, 2015
Tags
Pole sana wastara binadamu wengine hawana utu. Cjui ni kukosa malezi bora, wanazani We huumii watu wengine wabayaaaaa!!!
ReplyDeletemaskini, nimeumia na maneno yake...binadamu acheni hizo, kwani wastara naye ni binadamu, mumewe amefariki sawa lakini maisha inabidi yaendelee, mana kwanza bado ni binti, anahitaji kuwa na mwenzi. ila pia Tanzania matumizi yetu ya mitandao ni mabovu kupindukia, kama nia ni kujenga basi sisi watz asilimia 99.99% ni kubomoa. kutukana, kukashfu, kutafuta wa kungonoka nao, ndo tunavyovijua katika hii mitandao.tubadilike
ReplyDeleteforget and move on wasononeka every day
ReplyDeleteACHANA NAO !!!
ReplyDelete