Wema Amuumbua Kajala!


UBUYU: Gazeti la udaku la Amani, limeripoti kuwa mrembo na mwigizaji wa Bongo Movies ,Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi.

Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’

“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”

Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.
Wakati mwanahabari wa Amani akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.

Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.

Paparazi wa Amaani alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.

Mwanahabari wa Amani alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki huyo wa Kajala.

Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK,  mwaka jana walidaiwa kupatana lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wema acha usenge wee kumanina zako. Unavyomchukia Kajala wakati ww CK ulimuiba kwa mkewe.!! Malaya mbwa weee. Hata zile milioni 13 kwani asiejua nani kama ni za CK. Ww pale hukua na sent 5. Kutwa unajikwaza. Na nyumba ya kupanga na magari ya kuhongwa baada ya kusuguliwa kuma.Mwache mtoto wa watu. Unajifanya kushangilia watu kuyumba kiuchumi wakati ww mwenyewe huna hata muelekeo. Pumbaff mbwa koko weee. Haya endelea kubokolewa na Ivan na King Lawrence uone kama utapewa at least half of what Zari used to get. Una laana wee. Bora mzee Sepetu kafa hashuhudii umalaya wako tena. Nyoko weee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmhh! limekugusa eeh! Haya tuma salamu uchague na wimbo .......maana umetoa 'LAROHONI'.

      Delete
  2. Hivi hawa wadada wenzangu wanashindana nani amefilisika ani hajafilisika kwa lipi? Bora ushamba sometimes kuliko maisha ya namna hii. Kucha kutwa kaniibia bwana na bwana ni mume wa mtu. Hata aibu hawaoni?? EEh Mungu tunusuru sie tuliobaki yatupite kando.

    ReplyDelete
  3. Sasa bwana wa wema ni nani ? Maana team yake inampa kila mwanamme baada ya kumbwaga chibu list kubwa ni yupi tatizo elimu hawana bora elimu kuliko mali .mara zari mara kajala amebaki kutapa tapa pakushika hana

    ReplyDelete
  4. gazet kwaumbea kuchonganisha tuwatu achen wema hana mda wauoudaku wakipuuz muacheni mtoto wa watu du gazet amchok

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad