Polisi
mkoani Rukwa inawashikilia watu 17 wakiwemo waganga wa jadi 10
wakihusishwa na tukio la kikatili katika kijijini cha Kipeta , Bonde la
Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga ambako mtoto mlemavu wa ngozi (albino),
Baraka Cosmas (6) mwishoni mwa wiki alishambuliwa na kukatwa kiganja cha
mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana.
Miongoni
mwa watuhumiwa waliokamatwa ni watu saba ambao wanatuhumiwa kushiriki
katika kumkata kiganja mtoto huyo mlemavu wa ngozi akiwemo baba yake
mzazi, Cosmas Yoram (32).
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira amethibitisha
kukamatwa kwa watuhumiwa hao kufuatia msako mkali uliofanyika katika
vijiji vinne vya wilaya za Sumbawanga na Nkasi.
Aliwataja
waliokamatwa pamoja na baba mzazi wa mtoto huyo kuwa ni pamoja na
Mwendesha William (30), Masunga Bakari (50), na Ngolo Masingija (47)
wote kutoka kijiji cha Kaoze .
Wengine
ni Paschal Jason (40), David Kiyenze (45) na Mageta Shimba (46), wote
wakazi wa kikiji cha Kipeta , Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.
Kwa
mujibu wa Rwegasira, katika msako huo pia walikamatwa waganga wapiga
ramli chonganishi 10 akiwemo Sererino Kachingwe “Nakalango”(70), mkazi
wa kijiji cha Miangalua wilayani humo ambaye pia alipatikana na bunduki
aina ya Shot gun greener yenye namba G 73354 TZD,CAR 47478 ambayo
anaimiliki isivyo halali .
“Mtuhumiwa
huyu pia ni mganga wa kienyeji ambapo alikutwa na wanyama wawili aina
ya Kalunguyeye wakiwa hai pamoja na dawa mbalimbali za miti shamba.
"Pia
katika msako huo amekamatwa mganga mwingine wa kienyeji , Eliza Malongo
mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kijiji cha Kamnyalila akiwa na nyara
za Serikali, “ alieleza.
Aliongeza
Eliza alikutwa na ngozi ya chui, wanyama wanne waliokaushwa aina ya
Kalunguyeye na nywele zinazodhaniwa kuwa za binadamu pamoja na mfupa wa
swala.
Waganga
wengine waliokamatwa katika msako huo ni pamoja na Sodeli Malimbo
‘Chuchi” (69) mkazi wa kijiji cha Miangalua, Akobo Chinzwe (50), Leonard
Samson (59) na Engelbert Kasinde (45) , wote wakazi wa kijiji cha
Kamyalila.
Katika orodha hiyo wapo Boniface halya (49) na Julius Simbamwene (40) wote wakiwa wakazi wa kijiji cha Mpui .
“Watuhumiwa
hawa walikutwa na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli vikiwemo vioo
viwili, pembe moja, ndege na wanyama ambao hawakuweza kutambulika mara
moja, mizizi ya aina mbalimbali na dawa mbalimbali za kienyeji,“ alieleza Rwegasira.
Akifafanua
zaidi, Rwegasira alidai kuwa msako huo pia ulifanyika wilayani Nkasi
ambako alitiwa nguvuni mganga wa kienyeji aitwae Charles Misalaba (47) ,
mkazi wa kijiji cha Kacheche ambapo alikutwa na yai la mbuni , kucha za
chui , pembe ya korongo , ngozi ya paka pori na kobe aliyekaushwa.
Amesisitiza
kuwa msako huo bado unaendelea na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali wa shauri lao kukamilika.
Kwa
mujibu wake msako huo unafuatia watu wasiojulikana kumshambulia na
kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha
kutokomea nacho kusikojulikana usiku wa kuamkia Machi 08, mwaka huu.
Tukio
hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani
Sumbawanga, ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32)
na Prisca Shaaban pamoja na watoto wengine wawili ambao nao ni albino
wakiwa na umri wa miaka nane na minne.
Alisema
tukio hilo ni la saa nane usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo
akiwa amelala na mama yake. Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo.
Akielezea
zaidi, Kaimu Kamanda Rwegasira alisema usiku huo kikundi cha watu
wasiojulikana walivamia nyumba alimolala Baraka na mama yake mzazi,
Prisca wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo mapanga na fimbo na kuanza
kumshambulia kwa kumcharaza viboko Prisca baada ya kukataa kuwapatia
mtoto huyo, mwenye ulemavu wa ngozi.
“Baada
ya kuingia ndani ya nyumba hiyo walimwamuru mama mzazi wa mtoto Baraka
kuwakabidhi mtoto huyo, lakini alikaidi ndipo walipoanza kumshambulia
kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumjeruhi
vibaya …
“Waliingia
ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika
hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia
na kuondoka nacho kusikojulikana,” alibainisha.
EEE MUNGU TUKUOMBA UTUONDOLEE LAANA HII YA KUWAUA HAWA NDUGU ZETU MAALIBINO. MUNGU TWAKUOMBA UWALINDE WATU HAWA!!!!
ReplyDeleteWatanzania tunazidi kumchukiza Mungu kila leo,Mauaji,rushwa, N.K.
ReplyDeleteTusubiri gharika tu.
JAMANI BABA BABA NDIO UNAMUARIBU MWANAO NAMNA HIII?? JAMANI AKINA BABA MAALIBINO WOTE WACHUNGUZWE MAANA MATUKIO YOTE AKINA BABA WANAHUSIKA!!!!
ReplyDelete