Aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA Zitto Kabwe Amepokewa Rasmi Ndani ya ACT..Yametiamia

Hayawi hayawi… Sasa yamekuwa! Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.

NB: ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbe zile mbwembwe zoooote ni za kuishia kujiunga na hicho Chama feki feki hahaha hahaha aaaaaaahhhhh

    ReplyDelete
  2. hana lolote huyu, aende zake, tatizo la huyu jamaa anatamaa sana na madaraka, ovyo kabisa huyu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad