Askofu Wa Kanisa Katoliki Amjibu Migiro....Asema Viongozi Wa Dini Wana Haki ya Kuwaambia Waumini Wao Kupigia Kura Ya HAPANA Katiba Inayopendekezwa

Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge mkoani Kagera, Seveline Niwemugizi amesema, viongozi wa dini wana haki ya kuwaelimisha waumini wao waweze kujua kinachoendelea wanapoona kuna mambo hayaendi sawa katika jamii.

Niwemugizi alisema pia wanayo haki ya kuwaambia waumini wao kuipigia kura ya Hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo.

Akizungumza na gazeti  la  Mtazania, askofu Niwemugizi, alisema wao kama viongozi wa jamii hawawezi kuona waumini wao wanapotea halafu wanakaa kimya. Kufanya hivyo kutasababisha waingie kwenye uovu, alisema.

Askofu Niwemugizi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kuwataka maaskofu wasiwafundishe wananchi jinsi ya kupiga kura bali wawaache watumie haki yao ya katiba kupiga kura kulingana na utashi wao wenyewe.

Sisi ni viongozi wa dini hatuwezi kuwaona kondoo wa Bwana wanapotea halafu tukakaa kimya au kuwaacha, tutakuwa hatujatenda haki, lazima tuwaambie waweze kuondoka kwenye kundi hilo na waweze kujitambua,”alisema askofu huyo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).

Alisema hata viongozi wa serikali wanawaambia wananchi waipigie kura ya NDIYO, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inalinda masilahi yao na kuhoji haki hiyo ya kuwaelekeza hivyo wananchi wameipata wapi?

Nimeshangaa kusikia kuwa Waziri anasema viongozi wa dini hatuna haki ya kuwaambia waumini kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, mbona Serikali imewaambia wananchi waipigie kura ya ndiyo, haki hiyo wameitoa wapi,” alihoji.

Juzi, Waziri Migiro aliunga mkono kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye aliwataka viongozi wenzake wa dini kuacha kuwafundisha waumini kupiga kura ya hapana, bali waumini hao wanapaswa kufanya uamuzi wao kwa utashi wao wenyewe.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wanasiasa wanashauri na kusisitiza tupige kura ya 'NDIYO', kwanini wao hawasemi tufanye uamuzi kwa matakwa yetu, kwa upande wao ni sawa maana kila muwamba ngoma ngozi huvutia kwake. kama kuna kundi ndani ya jamii ambalo linaona mambo hayaendi sawa lina haki ya kukemea na kusema 'HAPANA'.

    ReplyDelete
  2. KAMA VIONGOZI WA DINI HAWANA HAKI YA KUSEMA TUPIGE KURA YA HAPANA NA SERIKALI NAYO HAINA HAKI YA KUSEMA TUPIGE KURA YA NDIO!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maaskofu wana haki ya kuelimisha jamii waonapo kondoo wao wanaenda pospotakiwa.

      Delete
  3. Mi c kondoo...we kumbe kondoo...achen kufanya viongoz wa din kama miungo watu.muwe Na maamuz yenu wenyewe

    ReplyDelete
  4. Maaskofu njaaa tuu inawasumbua,ngoja Mwigulu akate misamaha ya kodi kama ilivyokua kwa Mkulo uone watakavyolegea kama wamepigwa baruti!
    Ndio maana Pengo kawaona hawana akili na ni uzoba kumchagulia mtu maisha yake wakati wao kuoa hawataki lakini wanawaambia waumini waoe,si ushamba huo!

    ReplyDelete
  5. Kila mtu ana maanuzi yake kama wewe si kondoo wa bwana sawa kapige uanvyopenda wewe hiyo ni haki yako, hujalazimishwa kufuata wanayosema viongozi aidha dini/serikali

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad