At The End Fahari ya Mwanamke ni Mwanaume...Mambo ya Kujisifia U Single Mother ni Mbwembwe tu ila Moyoni Inakusuta

Nikakumbuka mada nyingi zilizowahi kutolewa hapa kutetea single parent family nikaanza kuzitafakari na kuona hazina ukweli wowote na kwamba kwa namna moja au nyingine zinapotosha kizazi hiki cha sasa.

Naturally, a female should be possesed by a male hiyo ndio fahari na usalama wake kutokana na alivoumbwa na mwenyezi Mungu. Mwanamke anasikia fahari, protection na safe sana akiwa na mume around, Haya mengine ni kujifariji tu hakiyanani.

Msipotoshe jamii kwasababu katika ujana mlikosea na kajikuta nje ya qualification za kuwa na familia yenye baba na mama kwa pamoja. Au kwsababu ya matakwa fulan fulan usipotoshe jamiii kuwa single parent family ndio mpango. Maana kwa upande mwingine that is selfish.

Beijing things and technology ni kati ya vyanzo vya kuwafanya wanawake wengi wajifariji kuwa inawezekana kuwa na familia zao bila kuhitaji wanaume but ukweli unabaki palepale kuwa wanawahitaji wanaume. Tusiendelee kuharibu jamii, kama uliharibu na ikashindikana kuishi na mwenza wako basi jitahidi watoto ulionao kuwaambia ukweli sio kuwajengea chuki kuhusu mzazi mwenzio na wakajikuta wanachukia ndoa. Madhara yake ni makubwa kuliko unavojifurahisha kwa kauli unazowapandikizia watoto wako.

Turudi katika lengo la Mungu kumuumba Adamu na Eva ambalo ni kutengeneza couple itakayotimiza makusudi ya Mungu kwa kusaidiana lakini pia kuzaa watoto watakao lelewa na wazazi wao.

GOOD MORNING!

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani umenifurahisha sana....hapo ndio huwa hata nakinzana na marafiki zangu kuhusu kuwa na mume...wengi wameshakosea tangu ujanani kama unavyosema ila sasa hivi wanajifariji sana kwa kujiita single parent..hiyo tabia imeibuka sana kwa wanawake wa siku hizi wakidai hawataki manyanyaso ktk mahusiano sasa najiuliza mama zetu waliwezaje kuishi na baba zetu mpaka wakazikana na walitulea wakiwa wawili....hebu wanawake ambao hamjaolewa acheni hizo tabia za kuiga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Poza Koo kwa Mangi mdau,
      nakuja kulipa.

      Delete
  2. midume ya siku izi inakimbia majukumu why usijiite single parent wajat mtoto ni faraja ukae msubili baba anayekimbia majukumu mala akianza mausiani na ww eti unafanya kazi gan ili umlee tu acheni kukimbia mjukumu la sivyo single tutakuwa wengi sana

    ReplyDelete
  3. Hmmm, msiwadanganye wenzenu, hao wanaume wengine ni stress tupu tu, kila kona, waweza kuta ana milolongo ya michepuko wachaa, pombe pombe yeye, nyumbani wala haudumii, bali ni matatizo tu, sasa hapo si mzigo tu huyo wa nini? kama single mamy unajimudu, Angalau si wote, lakini wapo, baadhi yao wenye tabia kama hizo

    ReplyDelete
  4. Ndoa ni Baraka kwa badhi ya watu na Ndoa ni ndoana pia kwa baadthi ya watu,, ni heri kuishi single mother kuliko kukaa kwenyendoa ndoana unaumia unateseka uko na majonzi kila sikuili ku keep status kuwa uko kwenyendoa, kwa wale ambao ndoa kwao ni baraka waendelee kumuomba mungu ndoa idumu na amani itawale, ila kwa wale ambao ndoa ni ndoana usiohope kuwa single mama, as long as ur happy, Usii ishi watakavyo Ishi utakavyo, Salute kwa Single mama na Salute kwenu mlio kwenye ndoa ndoana mnavumilia kwa kuogopa ukitoka watu watasema nini!

    ReplyDelete
  5. Wanawake wasikuizi hamna uvumilivu mnalinganisha urafiki na ndoa ndiyo tatizo huo usingle parent una effect kubwa kwa mtoto aliyeweka baba na mama anaakili mno ila nowdays viseversa is true mpo wrong ndoa ni ndoa na urafiki ni kitu kingine tofauti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndoa ni nini na urafiki ni nini? hebu elezea acha kutuletea theory zisizo na kichwa wala miguu, ndoa ni mateso na urafiki ni raha au?

      Delete
  6. Tatizo kuna watu wanachonga wanaona kila siku wanawake ndio wakorofi kumbe wanaume wengi ndio kisa nasababu hakuna mwanamke atakae acha nyumba yake km atapatiwq huduma nzuri yeye nawatoto wake unajikuta mwanamke unahangaka mwanaume haoni kisa mchepuko adabu hana ndani yanyumba etii nivumilie tunavumilia utopolo...zaman wazee wetu wakiwa navimada wanafanya kwaheshima mpk mnaletewa ndugu zenu mijitu mizima lkn sasa shida tupu kila mtu aishi vile anawez tusitazame watasema nini baba wengine wa traumatised watoto wakwanz

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad