Baada ya Kuhamia Nyumba Mpya, Diamond na Zari Roho Mkononi, Yabainiki Kwake ulinzi ni Sifuri, Mwenyewe Akiri Kuishi kwa Hofu

TAHADHARI ichukuliwe! Habari zikufikie kuwa, baada ya staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz‘ na mpenzi wake, Zarinah Hassani ‘Zari’, kuhamia kwenye mjengo wake mpya uliopo Madale jijini Dar, imebainika kuwa familia hiyo inaishi roho mkononi kufuatia ulinzi sifuri, jambo linalowafanya kuishi kwa hofu tupu

Kikizungumza kwa hofu juu ya familia hiyo, chanzo chetu makini kilipasha kwamba, pamoja na Diamond kutumia mamilioni ya fedha kujenga nyumba hiyo ya gharama kubwa, sasa changamoto imehamia kwenye ulinzi na usalama wao

“Jamani watu wanampongeza Diamond kwa kuhamia nyumba mpya lakini wale jamaa aisee wanapaswa kuombewa kila kukicha.

“Pamoja na kushusha mjengo wa maana bado changamoto ni juu ya ulinzi wao.

“Huwezi kuamini Diamond bado anaishi kizamani sana na sijui kwa nini anajiamini kiasi hicho wakati anajua wazi kuwa yeye ni staa wa Afrika na hapaswi kuishi kwa ulinzi hafifu.

MAENEO HATARISHI?

“Nasema hivi kwa sababu hata maeneo anayoishi ni hatari sana kwake hivyo anatakiwa kuwa na ulinzi mkali ili tu siku moja asije akafanyiwa kitu ambacho taifa likaingia kwenye hasara ya kumpoteza nyota mkubwa kama yeye.

“Nina uhakika asilimia mia moja Diamond hadi leo hajaanza hata kufanya process (taratibu) za kuchukua silaha (bastola).

“Mimi naijua vizuri Madale ni sehemu ambayo watu huwa wanavamiwa mara kwa mara na wanaishi kwa hofu kama Diamond anavyoishi.

HIKI NDICHO KINACHOMPONZA

“Kitu kingine kinachomponza Diamond ni ishu ya kuweka kila kitu kilichopo ndani kwake mitandaoni. Usione kila mtu anasifia lakini kuna wengine wanavitolea macho.

“Kwa mfano katupia picha za toilet (choo) ambacho kimepakwa dhahabu na kusema kimegharimu shilingi milioni 70.

“Hajakaa sawa akatupia picha za jikoni kwake kuna vitu vingi vya thamani kubwa kila mahali mpaka kwenye korido kuna flat screen (runinga). Huko si ni kuwakejeli watoto wa mbwa? Ni vizuri akaacha kufanya hivyo kwa sababu anawapa watu tamaa,” kilitiririka chanzo hicho.

ANA ULINZI GANI?

Juu ya ulinzi wa nyumbani kwa Diamond, chanzo hicho kilidai kwamba, mbali na baunsa anayewalinda aitwaye Mwarabu hakuna askari wa silaha anayelinda nyumbani hapo hivyo jamaa anatakiwa kufanya haraka kuajiri walinzi wenye silaha.


Baada ya habari hizo na uchunguzi wa kutosha, Ijumaa Wikienda lilimsaka Diamond a.k.a Dangote au Chibu ili kujua namna anavyoishi na jinsi anavyoimarisha ulinzi wake na familia kwa jumla.

Diamond, mbali na kukiri kuwa na hofu, alikuwa na haya ya kusema: “Suala la ulinzi wangu nalijua mwenyewe lakini zaidi watu wanatakiwa kujua mimi nipo na mlinzi na ninaendelea kuimarisha ulinzi wa nyumbani kwangu.

“Sidhani pia kama ni suala zuri sana kwa watu kujua siri za ulinzi wangu ila mambo mengi ya kujilinda niko kwenye michakato ya mwisho kukamilisha na soon (haraka) mambo yote yatakaa levo maana huwezi ukafanya kila jambo kwa wakati mmoja,” alisema Diamond huku akikubaliana na ushauri wa gazeti hili juu ya kuongeza ulinzi alionao wa baunsa.

ILIWAHI KUMTOKEA SUGU

Huko nyuma iliwahi kumtokea Mwanamuziki Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) ambapo alikuwa amerejea kutoka nchini Uingereza.

Akiwa amepanga nyumba nzima maeneo ya Tegeta, Dar, Sugu alifanyiwa makala ya runingani na kuonesha vitu vya thamani vya nyumbani kwake.

Siku chache baada ya kipindi hicho kuruka runingani, jamaa huyo alivamiwa na kuporwa kila kitu lakini yeye hakudhurika.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wanavyo sema Mjengo nikajua BOoNgee ya MjuMba...kumbe ni nyumba ya kawaida hivyo....uswahilini...khaa waandishi bwanaa......

    ReplyDelete
  2. Waandishi wanapenda kufanya story kuwa kubwa kwa sababu wanatafuta umaarufu, Kuhusu Diamond nampa hongera kwa kufikia hapo alipo, sio mjumba wa kutisha kama wasemavyo waandishi mbuzi wa udaku, hawa udaku hawafai hata kidogo na habari zao sio za kuzifuatiliza naa kuzitilia maanani

    ReplyDelete
  3. Du sasa kila mtu akisema aoneshe Mali zake hapa si mutakimbia mji

    ReplyDelete
  4. yeah, when you put yourself out there, what do you expect???? kuna watu hawajua hate chakuna cha jioni watatoa wapi na were unakaria chop cha millions do you think the gonna like it???? nooop. sometime is good to keep things for yourself and private. kana wamtu wana mpaka private jet tanzania na huwasikii wakivinadi, najua watt ambao nimatajiri hapo bongo ambao wanaingiza up to one million us dolla na hata sikumoja sijawahikuona wanadi what the have out there. Na mke wake hula anakeep very lower, hakuna mashauzi.
    so please people keep it for yourself.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama msanii lazima ujinadi kujiweka sokoni....mashabiki tunapenda kuckia wasanii wana maisha tafauti hiyo inanifanya nilipi kiingilio kikubwa kumuona.....sasa kama hajitangazii ofcoz thamani yake inashuka....kama siasa vile...iyo ni marketng strategy.. jombaaa

      Delete
  5. Aaaah! Hizi ni story za uzushi na udaku wa mjini! choo cha million 70???? alafu mjengo wenyewe uko uswahilini. udaku wanajua kweli kuzusha,, story za namna hii zinaweza kufanya jamaa anavamiwa na majambazi wakizani eti ana vitu vya samani kumbe wala

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad