Bifu la Lady Jaydee na Madam Ritha wa BSS

Katika kusheherekea sikuuu ya mwanamke Duniani, Mwanamuziki mwenye hadhi ya kipekee bongo, Judith wambura mbibo maarufu kama Lady jaydee ame share story yake fupi kuhusu bifu lililowahi kutokea miaka ya nyuma kati yake na Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha.

Akitiririka kwenye ukurusa wake wa Instagram, staa huyo ambaye hana mpinzani ndani ya Bongo Fleva, alikiri kutofautiana na mwanamama huyo, baada ya madam ritha kumpaka make up lady Jaydee ambapo Jide alikuwa akiifuta hali iliyompelekea Madam kumgombeza hali iliyozua tafrani kwa mwanamuziki huyo, na kusababisha ugomvi ambapo bifu hilo lilidumu kwa mda Wa miaka mitano bila mastaa hao kuongeleshana wala kusalimiana.

Hata hivyo staa huyo amekiri kumaliza tofauti yake na mwanamama huyo kwa kudai ulikuwa ni utoto na sasa hivi bifu kati yao limeisha.

Source: Lady Jaydee

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA JIDE KWA KUMALIZA TOFAUTI NDIO INAVYOTAKIWA!!! BIG UPO

    ReplyDelete
  2. Ana mabifu na watu huyo balaa, Ruge, mwana FA, mumewe, nk

    ReplyDelete
    Replies
    1. MNAFIKI WEWE !!! WEWE HUNA BIFU NA MTU??????? WIVU WAKO TU

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad