Bongo Movies Hili la Ukimwi Mlitazame Kwa Jicho la Tatu

Kwenu mastaa wa Bongo Movies, bila shaka mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Nawapongeza kwa hilo maana kazi nzuri tunaziona kila kukicha.Mkitaka kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya, kama kawaida naendeleza harakati zangu ndani ya mjengo wa Global Publishers.

Leo nimewakumbuka kupitia barua sababu wengi wenu huwa hatupati muda wa kuzungumza. Naamini kwa barua hii ujumbe utawafikia wengi kwa wakati mmoja.Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwakumbusha kuhusu suala zima la ugonjwa wa Ukimwi (Ngoma). Hakuna asiyejua kwamba ugonjwa huu ni hatari na unaua.

Ndugu zangu, nimeguswa kuwaandikia barua hii sababu ukweli ni kwamba aina ya maisha yenu wengi wenu nayajua. Mara kwa mara tumekuwa tukisoma kuhusu nyinyi kushea mabwana na mabibi kwenye magazeti yetu.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.

Kwa nini msifanye kazi zenu za kuigiza ambazo zimewapa umaarufu. Sanaa si ndiyo imewafanya muwe maarufu? Kwa nini mnaamua kuiweka kando?Hamtaki kufanya kazi, mnataka kugombea mabwana wenye nazo. Mbaya zaidi mabwana wenyewe mnaowagombea ndiyo walewale, fulani anamuona mwenzake anatembea na mtu fulani basi na yeye anamzunguka kwa tamaa ya fedha.

, Nasibu Abdul ‘Diamond’Hata huyo anayemzunguka mwenzake naye inafika wakati anapokonywa na mtu mwingine. Katika mzunguko huo mmoja akiwa muathirika basi wote mmekwenda na maji.

Baadaye msururu wa mabwana unahamia kwenda kwa mastaa wenzenu wa filamu, nao kila kukicha mnabadilishana. Leo utasikia fulani anatembea na fulani kesho amehamia kwa mwingine.Mastaa wa kiume wanatumia kigezo cha kudai watawachezesha sinema wasanii wachanga, ngono zembe inatawala, hakuna tena kuwapa hata hizo nafasi za kuigiza.

Jamani katika ulimwengu huu wa sasa si wa zama zile. Watu wanapaswa kubadilika, kuishi kisasa, kujitambua afya na kujikinga.Elimu imetolewa ya kutosha, hakuna mtu asiyejua. Kwa nini muendelee kufanya ngono zembe wakati mnatambua madhara yake? Kwa nini tunayahatarisha maisha yetu kiasi hiki? Tubadilike!

Mastaa wa kike badilikeni, fanyeni kazi msitegemee mabwana. Watanzania waliwajua kupitia sinema na michezo ambayo mlikuwa mkiigiza, komaeni kupitia kazi hizo za sanaa muweze kutengeneza kazi nzuri ambazo mtaziuza ndani na nje ya nchi.

Tumechoka kusikia habari za kukwapuliana mabwana. Tuseme inatosha kufanya ngono zembe.
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!

Barua Nzito By Erick Evarist, Global

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli tumechoka jamani fanyeni kazi zi sadifu uafrika kila kitu kuiga mpaka hamueleweki tena na mbaya zaidi hiyo mizungukano yenu kama kuku au bata bandani ndo inachosha kwasababu wengi wenu tunawaona wakienda kuchukua tembe zetu zile sasa mnataka kufa wegi au mfe kwa mkupuo jamani mashabiki hatutalia tena mjipange kwa kweli epukeni vitu vya ajabu ajabu wengine rudini shule maana mnaonyesha udhaifu mpaka basi......pia global na magazeti yenu embu badilini ramani ataye fanya kitu chema ndo mumuandike hayo maovu achaneni nayo itawaonyesha ujinga wao hadharani nawatabadilika naapia vile jaribuni tuu mtaona... hata Hollywood kuna uozo ila huu wa bongo muvi umezidi unawadudu ndani mwake...nimefurahi ulivyo wakumbusha kwa kweli kaa kidogo waeleze hasara za mikorogo kwa jinsia zote nashukuruu.

    ReplyDelete
  2. wacheni wafe, nanyie hangalieni maisha yenu sio mnawasema mastaa wakati nanyie wenyewe mko kwenye mkumbo huo wa kutafuta ustaa. manake ustaa wa Bongo ni kulala na staa ili uwe staa... foolishnes

    ReplyDelete
  3. Sijaelewa diamond kaingiaje hapa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad