ZITTO KABWE |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe, licha ya yeye kuwa ndio 'the most active MP of all time!', kwenye bunge la sasa, leo ameweka historia nyingine kwa kuwa ndie mbunge wa kwanza kung'atuka rasmi ubunge kwa kuaga rasmi kwa barua na kisha kulihutubia Bunge kuliaga!.
Hatua hii, sio tuu inamfanya Zitto kuendelea kuwa shujaa, bali pia kwa hatua hiyo, ameipiga Chadema bao la kisigino, kwa sababu sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema na sio Chadema imemfukuza!.
Uanachama wa chama cha siasa, hauombwi kwa kauli tuu bali kwa maandishi ya kujiandikisha uanachama, na kufukuzwa rasmi kwa uanachama, haufukuzwi kwa kuitishwa press conferences, kusema fulani sii mwanachama wetu, bali hufukuzwa kwa barua, hivyo mpaka hapa ninapoandika, Chadema ilimfukuza Zitto kwa kauli tuu ambayo sio kufukuza rasmi, lakini kwa barua ya Zitto, hii sasa ndio barua rasmi ya uthibitisho kuwa sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema!.
Ama kweli Zitto ni shujaa sijaona mfanowe!.
Hii ni threadi ya angalizo kwa Chadema na wapenzi wake, msishangilie sana hadi mkajisahau, wekeni na akiba japo kidogo ya aftermath ya kung'atuka kwa Ziito kwa sababu, kujiuzulu huku kwa Zitto, mnaweza kukuhesabu kuwa sasa ndio mwisho kabisa wa kirusi chenye jina la ZZK, and you have closed the chapter and move forward!, bora jiandaeni kabisa!, kunaweza kusiwe ndio mwisho bali sasa ndio mwanzo wa series za 'karma' effects ambazo ama zitamtandika Zitto mwenyewe kama kweli ni msaliti, ama zitaindandika Chadema, bila huruma, kama ni kweli Chadema haikumtendea haki!.
Kwa mnaoijua 'karma', shangilieni kwa kiasi tuu!, msimbeze, msimdhihaki wala msimtukane kwa sababu hakuna mkamilifu. Zitto alikuwa mwanachama wenu, hakuwabeza, hakuwatukana amewaaga rasmi kwa heshma, nanyi mnategemewa mtairudisha heshma vile vile!.
Nashauri wale msio jua "karma" ni nini, jipeni homework kidogo tuu, kisha ndio mje kuchangia!.
Nitazijibu hoja zote za msingi, ila kwa wale vichwa maji na madebe matupu, mtanisamehe, nitawashukuru tuu kwa kuchangia uzi wangu.
Pasco.
Note to mode: This is opinion article na sio reportage!
Kweli wewe ni kichwa maji kabisa, kati ya Chadema na Zitto na kaacha mwenzake? huna akili wewe Katiba ya Chadema kama umeisoma haungeleta ujinga huu,
ReplyDeletehuyu alishafukuzwa muda mrefu na Chadema ipo palepale, sasa ndo itaanguka leo!! wewe mwandishi vipi!
ReplyDeleteNdugu Admin sijui unaposema Karma una maana gani kwa kuhusisha na hili suala. Ni kweli CHADEMA waliitisha Press Conference na kuzungumzia mstakabali wa aliyekuwa mwanachama wao kufuatia hukumu ya kesi ambayo ni yeye huyo huyo mwanachama aliifungua pale Mahakama Kuu. Na of course CHADEMA walilizungumzia kupitia mwanasheria wao. Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini huyo mwanachama asingesubiri hatua za kiofisi za kichama zichukue mkondo wake??????. Ni kwa nini asingesubiri akabidhiwe barua yake itakayoonyesha ukomo wake wa uanachama wa CHADEMA kabla ya kukurupuka kwa kwenda kuliaga bunge????????. Sasa hiki tunachokiona ni kiherehere cha huyo mwanachama, kwanza ni kwa kutotaka kusubiri itikadi za Chama zichukue
ReplyDeletemkondo wake na pili pengine ni pamoja na kutafuta sifa za kisiasa zisizokuwa na msingi. Lakini kwa mtaji huo unategemea utapataje hizo sifa kwa kutoonyesha subira na wala kutozingatia itikadi za Ki Chama??????? Natumaini Ndugu Admin utanipatia Black and White za hii issue na pia utanieleza kwa ufasaha bila kupinda maelezo ya kwa nini huyu mwanachama ameshindwa kusubiri itikadi za Chama zichukue mkondo wake!!! Nakushukuru sana!!!
But all in all huyo ndio Zitto Kabwe. Zitto mtaka misifa!!
Ndugu Admin acha kutuchekesha. Kumwita Zitto Kabwe eti ni "The Most Active MP Of All Time!" ni kichekesho na pia ni dhihaka kubwa sio tu kwa Bunge letu tukufu la Muungano wa Tanzania, bali pia hata kwa wananchi wa Taifa hili. Nakuomba utueleze ni Most Active MP of All Time in which comparison???? Ndugu Admin wa hii Blog, sisi wafuatiliaji wako tunaamini utakuwa unatuletea vitu sahihi na vya uhakika bila ya kupinda pinda ukweli wa mambo. Ni hayo tu!!
ReplyDeleteMuheshimiwa naona ume panic tuu, ukweli ipo pale pale kuwa Zitto alikuwa the most active MP compared to Lema, Mbowe, Mnyika, Sugu sababu wao walikuwa wanasubiri Zitto awaletee ideas then wao walete migomo bungeni badsla ua kutafuta suluhu.
DeleteJipimeni nguvu 2015 election ishafika achanI maelezo mmeshayatoa sana.
mwandishi bwege
ReplyDelete