Exclusive: Cheka azungumzia kifungo chake nje baada ya kutoka jela

Bondia wa ngumi za kulipwa duniani, Francis Cheka (32), amebadilishiwa kifungo chake cha miaka mitatu jela alichohukumiwa awali na sasa kuwa kifungo cha nje.

Akizungumza na Bongo5 leo, Cheka amesema tayari ameanza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro.

“Nawapenda sana mashabiki wangu, wazazi wangu, ndugu jamaa na marafiki kwa kuniombea na kunipigania mpaka sasa,” amesema. “Nashukuru kwa kunusurika kwa kifungo ambacho walikisikia awali lakini sasa hivi natumikia kifungo cha nje na tayari nimeshaanza. Namuomba Mungu mambo yaende vizuri ili kila kitu kiwe sawa.”

“Kifungo ni kifungo kwa sababu kipo kisheria naitumikia jamii, kwahiyo nitakuwa nafanya kazi za kijamii, kama kazi za usafi, mabarabari, kwa mkuu wa wilaya, na sehemu mbalimbali. Ninahitaji kutekeleza kama nilivyoelekezwa kisheria ili kiwe kizuri zaidi. Kwa sasa hivi niko vizuri zaidi ila kwa mchezo bado kwa sababu mpaka niachiwe huru zaidi. Mashabiki wangu watarajie kuniona baada ya kumaliza hukumu hii,” ameongeza Cheka.

Kwa upande mwingine, Cheka amesema ni mengi aliyojifunza kupitia kesi yake lakini kikubwa ni tatizo la watu kutoheshimiana.

“Napenda kukwambia kuwa bila kuondoa umwinyi Tanzania watu tutashindwa kuheshimiana, hakuna anayeweza kumuogopa mwenzake. Tunatakiwa kutimiza kile tulichoagizwa, hakuna mfanyabiashara duniani anaweza kukubali kufanya biashara ili apate hasara, wote tunataka tupate faida ili tuweze kuendesha maisha pamoja na biashara. Tunatakiwa tuheshimiane wenyewe kwa wenyewe. Watu ni wababe kwa sababu kuna vitu wanajivunia, sasa tukiendelea kwa hali hii hatutaweza kuheshimiana kabisa. Mtu anaweza akatumia cheo chake kumkoMOa mtu kwa shinikizo la mtu. Mimi ninachotaka kusema ni tuheshimiane na tufanya yale tuliyokubaliana.”

~Bongo5

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad