Mambo matatu aliyoyasema Jerry Murro kuhusu sakata la mchezaji wa Simba Ibrahim Ajibu.

Jerry Muro: “Mchezaji Ibrahim Ajibu tumebaini ana kadi nne za njano alizoonyeshwa katika mechi dhidi ya Stand United FC Uwanja wa Taifa Oktoba 4, Polisi Moro FC dhidi ya Simba SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Februari 15, Stand United FC dhidi ya Simba SC Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga Februari 22 na Simba SC dhidi ya Prisons FC Uwanja wa Taifa Februari 28,” Muro amesema.

“Kutokana na tukio lenyewe kuwa la kidhalimu na lenye kutaka kurudisha nyuma maendeleo ya soka la Tanzania, sisi (Yanga SC) tunaitaka TFF kuingilia kati utata huu kwa kuipoka pointi 3 klabu ya Simba SC ilizozipata katika mechi namba 125 dhidi ya Prisons FC kwa sababu ilitumia mchezaji asiye sahihi katika mchezo usio sahihi kwa mchezaji husika.
“Pili, tunalitaka shirikisho litoe adhabu kali kwa viongozi wote wa Simba SC na mchezaji husika kwa kikiuka kanuni na taratibu za uendeshaji wa ligi.

“Tatu, tunamtaka Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, Fatma Abdallah Shibo, ajiuzulu kutokana na kupindisha sheria na taratibu na pia kupotosha umma wa Watanzania kuhusu sheria na kutoa kibali hewa cha kuruhusu mchezaji Ibrahim Ajibu kucheza dhidi ya Prisons huku akiwa na kadi nne za njano,” amesema zaidi Muro.
Chanzo,Shaffih Dauda.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muro,tuache na simba yetu miaka 800.

    ReplyDelete
  2. Hata mkimchezesha mtu mwenye red card poa tu Watu wakae kimya kwavile nyie ni simba? Mpira wa Miguu una sheria zake sio siasa

    ReplyDelete
  3. Hata mkimchezesha mtu mwenye red card poa tu kwavile nyie ni simba? Mpira wa Miguu una sheria zake sio siasa hii
    Mjonba

    ReplyDelete
  4. SIMBA MMECHEMKA MTAMCHEZESHAJE MTU ALIYELIMWA KADI NNE ZA NJANOO??? ACHENI UJANJA UJANJA SOKA HALICHEZWI HIVYO. MECHI BATILI WAZI WAZI!!

    ReplyDelete
  5. KWENDENI ZENU HUKO NA MITIMU YENU UCHWALA KAMA CHAMA CHENU TAWALA YANI HII NCHI NI VULUVULU KILA SEKTA LOOH NGACHOKA KBS

    ReplyDelete
  6. Yanga safari hii mmepata mwana habari makini kwa kweli.WANASEMA MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE APEWE.

    ReplyDelete
  7. Aisee bwashee wenzio wanauza maduka wewe unauza umbea.,hujui sheria za soka ila unazisoma tu kwa huelewi,umewekwa hapo wenyewe hawajui unaingizwa mkenge hufatilii unaropoka tuu.,zamu yako ya kung'oka yanga imekufikia we kwanza simba tu mamluki ila njaa yako ndo mana upo hapo..uliongea ngasa haidai yanga Leo club imemlipa deni lake huoni kwamba uropoka tu?hats issue ynyw huifuatilii kuielewa Leo ngasa anakuonaje su mchawi tu wewe ulitaka kuzuia hela take??halafu hujamyomba msamahaa aibu au kina see.,Leo unajidai unamjua Ajibu unaumbuka na hilo sass,hilo soka sio udaku wewe acha umbea Wako uleeee uliokuponza ukajiona utapeeendwa na watu nyooo kidogo uende hela acha UBWEGE unaingizwa Chaka.......,nakusamehe Leo jichanganye tena sass.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wewe uwe na uhakika na usemalo,Bado kidogo mtajua mbivu na mbichi,na muache kukalia ushabiki usio na tija,tunaharibu soka letu sisi wenyewe watanzania.

      Delete
  8. Sio umebaini UMEBAINIWA wanakuona bwege wenzako ht ujinga unaongea Tu bila kufuatulia mwenyewe,ona sass unavyoumbuka wao Wako kimya we ndo mshambenga,we Dogo sana uijui yanga wanazidi kukupotezea cvii yako kwa kudanganya watu hutaaminika tena ukirudi kwenye udaku km ule WA Mikuni unabahati wewe afu bado uachi unoko Wako,kazi za watu WA soka hizo.,unapayuka Tu..,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko dunia gani?kuna uongo au udaku kwa suala la mikumi,hata picha hukuona?poleeeeeeeeeeeeeeeee

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad