Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Wasema Mvua Iliyonyesha Shinyanga na Kuua Watu 42 ni TONADO


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Agnes Kijazi amesema mvua iliyonyesha Shinyanga na kusababisha maafa kwa jina la kitaalamu inajulikana kama ‘Tonado’, ni mara ya kwanza kutokea hapa nchini.

Kijazi alisema katika ofisi za mamlaka hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Wabunge ya Miundombinu, jijini Dar es Salaam.

 

Alisema utabiri waliokuwa wameutoa wa saa 24 ulionesha kutakuwa na mawingu mazito katika eneo hilo, lakini hawakutarajia tonado kunyesha kwa kuwa sio mfumo wa

kawaida kwa hapa nchini.

 

Kijazi alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi kumekuwa kukiongezeka matukio ya hali mbaya ya hewa hata ambayo awali yalikuwa hayatokei.

 

Alisema tonado, kitaalamu ni mawingu mazito yenye unyevunyevu yanapozidi uzito yanaanguka mabarafu, hivyo kutokana na mabadiliko hayo upepo mkali unaozunguka sio hali ya kawaida katika maeneo ya tropiki.

 

“Inabidi tahadhari ichukuliwe tunapoona mawingu mazito kuepusha maafa,”alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad