Viongozi wa Vilabu na mashabiki nchini wametakiwa kuachana na tabia za kutoa lawama kwa magoli kipa wanaofungwa magoli mbalimbali ikiwemo kuhama goli na hatimaye kuweza kufungwa.
Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Kituo cha Magoli Kipa nchini TGC, Peter Manyika amesema, katika mazoezi kipa anafundishwa na kutahadharishwa mambo mbalimbali hususani kulinda goli inapotekea hatari ya kufungwa.
Manyika amesema, mashabiki na viongozi wanapoendelea na lawama watakuwa wanabadilisha magolikipa kila kukicha kwani kila Golikipa anakuja na tatizo lake na suala linalotakiwa ni kufundishwa zaidi ili kuweza kufanya vizuri na wapo magoli kipa wanaofundishwa lakini wanafungwa aina ya magoli ambayo huzuilika.
Manyika amesema, Golikipa anakuwa amebeba jukumu la watu wote hivyo suala la kufanya makusudi ili aweze kufungwa katika mechi mbalimbali linakuwa ni gumu kwania anaamini kila mtu anamtegemea yeye awapo langoni.
--------------
Note:
good comments peter
ReplyDeletehaya mambo ya simba na yanga yanamambo mengi sana, yani kwanza hizi timu zamani zilikuwa hazikutanagi hovyo hovyo, zinakutana kwenye ligi au mashindano makubwa, sababu nitimu zenye lawama kila siku mmoja wapo ukifungwa kwamba ooh kipa, au mchezaji fulani katuuza!!!! mimi ningeona ili kutoa shari haya mashindano ya hovyo hovyo kama bonanza kukutanisha hizi timu yangeachwa sababu watu wanaonufaika ni wingine na wanaoumia ni wingine, sababu kwanza hata hizi hela za mechi hizi za bonanza haitangazwi ni ngapi imepatikana, kwahiyo ni watu wachache wanaonufaika nazo kijanja kabisa.
ReplyDeleteSasa hivi Simba naYanga ni siasa pia.
DeleteWATANZANIA MKITAKA SOKA LETU LIKUWE LA MAANA NA KUFANYA VIZURI SIMBA NA YANGA ZITOKE 5 BORA MTANIAMBIA LAKINI HIII SIMBA NA YANGA TUTAPIGA MACH TIME TU HATUENDI KOKOTE SANA SANA KURUDI NYUMA TU
Delete