Mastaa Saba Bongo Wanaoetembelea Magari ya Kifahari

Asilimia Kubwa ya mastaa Wa bongo wamekuwa wakionekana wakijivinjari katika mitaa mbali mbali wakiwa katika magari ya kifahari. Lakini ukichunguza utagundua kuwa wengi Wa wasanii hao siyo wamiliki halali Wa magari hayo. Baadhi ya mastaa wanaosukuma ndinga za bei Kali apa bongo ni.

1: DIAMOND PLATNUM
Mwanamuziki anayedaiwa kuongoza kwa kuwa na gari la bei mbaya zaidi nchini ni Diamond Platnums ambaye kwa sasa anamiliki BMW X6 ambalo linauzwa kwa thamani ya dola 62,850 za marekani karibu shillingi million 150 za kibongo.

2: LADY JAYDEE
Anayefuata ni mwanadada lady jaydee anayemiliki magari mawili ya kifahari ikiwemo Nissan Murrano alilonunua kwa thamani ya shilingi mil 60 miaka kadhaa iliyopita na Range rover E lenye thamani ya dola za kimarekani 60,000 sawa ni shilingi mil 100 .

3: AY
Nafasi ya tatu imeshikwa na rapa mkongwe Ambwene yesaya anayemiliki Vogue sports lenye thamani ya sh92 miliion.

4: MASANJA MKANDAMIZAJI
Huyu anamiliki gari aina ya Land cruiser lenye thamani ya shillingi mil. 75

5: MRISHO MPOTO
Namba tano inamilikiwa na mtaalamu Wa mashairi nchini, mrisho mpoto anayemiliki Toyota Prado new model yenye thamani ya shilling mil 65.

6: JACKLINE WOLPER
Kwa upande wake muigizaji jackline wolper anamiliki land cruiser Prado lenye thamani ya shillingi mil 65.

7: WEMA SEPETU
Nafasi ya saba inashikiliwa na mwigizaji wema sepetu anayemiliki BMW 545 yenye thamani ya shilingi million 56, pamoja Na Nissan murrano alilopewa Na aliyekuwa mchumba wake diamond lenye thamani ya shillingi mil 36.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jitahidi kufanya uchunguzi was bei bro, list yako sio kweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. UDAKU MNALIPUA KAZI FANYENI UTAFITI WA KUTOSHA

      Delete
  2. usituletee bei za magari used... ni LADY JAYDEE peke yake ndiyo ana gari brand new Range Rover Evogue, hizo zingine ni takataka tu zilizotupwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. ALAAA KUMBE JIDE PEKE YAKE NDO ANA KITU KIPYA BRAND NEW!! HONGERA SANA JIDE MIYE SIKU ZOTE NAKUFAGILIA KULA 5

      Delete
  3. x6 kwa bei haitangulii evoque. lady jaydee nambari moja

    ReplyDelete
  4. Inakuwaje dollar 62,850 sawa na 150 milion halafu dollar 60 iwe sawa na 100 milion? Inamana tofauti ya gari ya jd na nasib kwa dola ni 2,850 halafu kwa sh iwe 50 milioni...!!!!

    ReplyDelete
  5. umezingua sana yaan hata kupiga hesabutu tu umeshindwa acha habari za kizembe unalipwa ufanye kazi sio ulipue kazi

    ReplyDelete
  6. JIDE NAMBA MOJA WEWE MTOA POST MZUSHI SANA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad