Mjengo wa Diamond Wazidi Kuwa Gumzo Mjini..Thamani yake Yashtusha Watu Wengi

KUKAMILIKA kwa mjengo wa Staa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo gumzo zaidi ni kuhusu gharama halisi huku mkandarasi mmoja akikisia kuwa si chini ya sh. mil. 400, Risasi Mchanganyiko linakupa stori kamili.

Akiuzungumzia mjengo huo baada ya kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani umechukua nafasi kubwa, na ‘material’ yaliyojengea ni ya gharama.

”Ukitazama kwa makini, material nyingi zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea,” alisema mkandarasi huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.

Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. m

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SASA NYUMBA YA GHARAMA ALAFU UZIO UNAANGUKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa cha ajabu nini? Acha wivu ww anonymou 10:21. Uko sawa sawa na Wema. Sasa kawanunia wote walio attend white party. Na bado mwaka huu. Atazidisha dose ya unga. Ugumba kwenda mbele na kuolewa NO. Dungaembe linaolewa tangu lini?? Eti mume hewa hapendi publicity...hahahahahah.Mmefuliaje sasa??

      Delete
  2. Mafundi wamechakachua

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad