Nay wa Mitego Atoa Kauli ya Kuwachukiza Wanawake..Awatumia Kama Bahasha ya kumletea Watoto Kisha Tupa Kule

Mwanamuziki wa bongo flavor ajulikanaye kama Ney wa Mitego ametangaza kuwa baada ya kujipatia watoto watatu, hana tena mapenzi na mama watoto hao bali ana mapenzi na watoto hao.

Kwa kauli hiyo, ni sawa na mama watoto hao kuchukuliwa kama bahasha maana bahasha ikishafikisha barua, inakuwa haina umuhimu tena bali kinachofanyiwa kazi ni barua iliyokuwa ndani.

Binafsi kama mwanaume sikufurahishwa na kauli kama hii kwamba hataki mazoea na mwanamke bali mapenzi ni kwa watoto, na je kama si huyo mwanamama hao watoto angeweza kuwazaa mwenyewe.

Huu pia ni ujumbe kwa wale wenye tabia kama za huyu jamaa na pia wale wanaotelekeza mama na watoto wanaenda kutafuta mwanamke mwingine.

Mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote labda itokee bahati mbaya mmojawapo kafariki lakini unakuta mtoto anateseka, pimbi anadunda mtaani.

Je wewe unamwunga mkono Ney wa Mitego kwa kauli yake.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hilo liney c limbwiga tuu hilo bado halijamaliza kula ujana iko cku yake litajutraaaaaa!!!

    ReplyDelete
  2. Siri ya ndani Ni wenyewe wanajua, lazima Kuna sababu iliyoleta kutoweka kwa mapenzi yao

    ReplyDelete
  3. KWA HIYO HATA MAMA YAKE HANA FAIDA KWAKE SIO?? AU NAYE ALIACHWA NA BABA YAKO NDO UNALIPIZIA?? WATOTO WANAHITAJI MALEZI MAZURI YA BABA NA MAMA. ONA MFANO WA H BABA NA FLORA !!!!BINAFSI NAKUONA HUFAI KABISA KUMBUKA UNA MTOTO WA KIKE AKIJA FANYIWA HIVYO UTAJISIKIAJE?? AU WATOTO WAKO WOTE WA KIUME??

    ReplyDelete
  4. haaa !!!!! mma yake alishamtukana kwenye nyimbo zake anatakua na umuhimu nae ???? Huyo jamaa tatzo lake ni moja tu ulimi bhassss lakini atakuja badilika tu i hope that

    ReplyDelete
  5. Marioo huyo analelewa na wanaume wa mademu zake wala hana jipya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad