Ngeleja: Zitto Aliomba na Kupewa Milioni 30 Kutoka kwa Rugemarila

Mh. Ngeleja akiwa anahojiwa na baraza la maadili amesema Mh. Zitto Kabwe alipokea shilingi milioni 30. Akaongeza kuwa kama wanahojiwa waliopokea fedha na Mh. Zitto aitwe kuhojiwa na baraza hilo.

Pamoja na kutaja wafanyabiashara na mashirika yaliyowahi kumsaidia, Ngeleja aliwasilisha vielelezo vya misaada hiyo.

Pia ,aliwasilisha kielelezo cha tuhuma zilizowasilishwa bungeni na Kambi ya Upinzani na mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde dhidi ya Zitto kuwa alipokea zaidi ya Sh milioni 30 kutoka Tanapa, NSSF na kampuni inayohusishwa na akaunti ya Escrow ya Power Solution Limited (PAP).

Kwa mujibu wa Ngeleja, pamoja na tuhuma hizo dhidi ya Zitto kuwasilishwa bungeni na vielelezo na kutaka Zitto afikishwe mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Ndio maana nasema hata kama ningepokea msaada huo kutoka VIP Engineering haukuwa kwa ajili ya maslahi yangu kwa sababu ni utamaduni uliojengeka kwa kampuni duniani kote kutumia sehemu ya faida zao kusaidia jamii, lakini pia nisingekuwa mbunge wa kwanza kupokea msaada wa aina hiyo,” alisema.

Pamoja na utetezi huo wa Ngeleja, Cyriacus, alisema utetezi uliowasilishwa na kiongozi huyo, hauna mashiko kisheria.

“Amejitetea kwamba fedha alizopokea zimetolewa kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake, lakini si kweli kwa sababu nyingine alichangia Kanisa Dar es Salaam, kutokana na hili naomba apewe adhabu kali iwe fundisho,” Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Hamisi Msumi, alisema baraza hilo limepokea na kusikiliza pande zote mbili na litawasilisha uamuzi wake kwa mamlaka husika ambapo itajulikana endapo mbunge huyo atahitaji kujibu mashtaka yanayomkabili au la.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad