Polisi Yawashikilia Watu 15 Kwa Kosa la Kula Njama ya Kumtorosha Gwajima, Majina yao Haya Hapa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
29/03/2015
WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao hivyo waliwakatalia kuingia.
Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa kundi hilo.
Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa na Begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya PUMAChaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi, Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24, Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62, Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30, Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva, Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60, Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39, Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yani haya makanisa uchwara haya, they do all of shit behind the door
    Naanza kumuamini aliyokua anayasema mr. Mbasha it might be true. Karma is a bitch!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad