Prof. Baregu: Zitto ni mzigo, Anaponzwa na Kibuli cha Kujiona Hakuna zaidi ya Yeye.

PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”
Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”

Udaku Specially

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumekucha kusemana kumekucha kutoana akili

    ReplyDelete
  2. Nani asiyemjua Baregu.....? Ewe mtanzania amka sasa, mengi yataongelewa lakn daima yakuambiwa ongeza na zako.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad