Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano.
Pia,Rais Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu suala la katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana.
Rais Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam.
Chanzo: ITV
Tanzania sio nchi ya dini,na inaendeshwa na katiba
ReplyDeletekwa nini mambo ya dini fulani yakajadiliwe bungeni kwa ajili ya kuingizwa kwenye katiba?
sheria za dini zihusishwe na dini husika na sio kupelekwa bungeni.TATIZO LIKO WAPI WAJEMENI?