Siri Imefichuka:Rais Kikwete “Abariki” Mbio za Urais wa Lowassa

SIRI imefichuka. Mbio za Edward Lowassa, kusaka urais kwa udi na uvumba, zimebarikiwa kwa asilimia 100 na Rais Jakaya Kikwete.
Lowassa amekutana na Kikwete mara kadhaa na kufunga makubaliano ya siri yanayolenga kumsaidia yeye kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Yote yanayofanywa na Edward (Lowassa), yamebarikiwa na Kikwete. Bila hivyo, Lowassa asingekuwa na ubavu wa kufanya anachokitenda,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.
Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Jamhuri.
Kuibuka kwa taarifa kuwa Lowassa amefunga makubaliano na Kikwete, kumekuja katika kipindi ambacho mwanasiasa huyo aliyeapa kufia katika vita ya kuwania madaraka, ameanza kupokea makundi ya wananchi akidai wanamuomba kugombea urais.

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, “Kikwete na Lowassa wanakutana sana, tena kwa siri. Wamejadili mengi, ikiwamo kinyang’anyiro cha urais. Itakuwa ajabu, bwana huyu kutokuwa mgombea kupitia CCM.”

Waziri mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa kufua umeme, kati ya serikali na kampuni ya Richmond, tayari amefungulia anaowaita “wafuasi wake,” kushawishi baadhi ya watu kwa lengo la kutafuta kila upenyo kuhakikisha anapata nafasi ya kushika utawala Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu walio karibu na mwanasiasa huyo, makubaliano yake na Kikwete ndiyo yanayomfanya kuwa “mbogo” hadi kuikuka taratibu za chama chake.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu – kuchagua rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online anasema, pamoja na kuwapo makubaliano hayo, bado Lowassa hawezi kujihakikishia nafasi ya kuwa mgombea.
Anasema, Lowassa anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa makundi ya yaliyopachikwa jina la “wahafidhina” ndani ya chama chake.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Akiwa mgombea wa sisiem, basi huo ndo utakuwa mwisho wa chama hiki,, wasimkubali ili sisiem iendelee

    ReplyDelete
  2. huyo lowasa naye hamjui msanii alivyo aakavyomfanyaia usaiinii we hutaamini we subiri utacheki white house wana mtu wao tayari mrs msanii ndo mpango mzima subiri utaona kaa lowasa hajaama chama

    ReplyDelete
  3. Acheni ufukunyuku nyinyi@

    ReplyDelete
  4. Ee uongozi mtamu kweli kweli...yaani pamoja na kashifah ya wizi..mtu uliwa waziri ukajiuzuru..tena bado wataka kugombea urais..ktk nch hiyo hiyo karne hiyo hiyo!!!...Kiyamah kimekaribia..watu hata haya hatuna..Na huyo mweshimiwa rais kweli haoni haya.wala kumuogopa Mungu..mtu alikuwa waziri wako kisha kapata kashifa mbaya kama hiyo..ukamshawishi ajiuzuru..tena wewe wewee eti unamuunga mkono achukue nafasi yako!!!.hivi mnawaongoza wana wa Adam????au mnaongoza wana wa mbuzi????Muogopeni Mungu..Umauti unatungojea sisi sote..ni hayo tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.Kondoo wako akipotea na kisha ukampata,je hutamchanganya kwenye kundi la kondoo wako waliosalia na kuwalisha kwa pamoja?
      2.Akosae na kutubu husamehewa.
      3.Lowasa amefanya mengi mazuri mara baada ya kugundua alikosea,anastahili kwa sana kupewa nchi atuongoze.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad