Taasisi ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji ambao inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali itashindwa kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini ya kiislam popote walipo kuipigia kura yaHapana Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Kauli ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa na muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki (TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Baraza la Makanisa la kipentekoste(CPCT) ambao wote kwa pamoja waliwataka waumini wa dini ya kikristo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa kutokana na serikali kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
Akitoa tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam ambalo ni muunganiko wa taasisi za dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya habari jana Jijini Dar es Salaam, aliitaka serikali kuwachukulia hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchochezi.
“Serikali iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
Aidha, Sheikh Katimba aliitaka Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu mawili.
Mosi: Serikali iache njama na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.
“Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi” alisema Sheikh Katimba.
Pili: Serikali igharamie mahakama hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
“Na pia mahakama hiyo igharamiwe na serikali kama inavyogaramia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding (MOU) , mkataba ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema sheikh huyo
Mtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano
ReplyDeleteMtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano hebu waanze tuone
ReplyDeleteMtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano hebu waanze tuone
ReplyDeleteHawa ndo kabisa wameharibu, hawajui kitugani wanataka. Kwanza wao lazima wakubaliane kwamba wako chini ya BAKWATA!
ReplyDeleteMungu wetu iponye Tanzania tusaidie huku tunako elekea siko katiba inatusaidia wote inatengenezwa kwa manufaa ya kila mtu sio mtu moja unaposema wa kamatwe wamefanya nini wamekosea wapi lazima mtu anapopewa katiba aelwe nini anatakiwa afanye Mungu awape ufahamu msilete sababu zisizokuwa za msingi ambazo hazijengi nyie ndo mnaleta uchochezi mnaosema wakamatwe kwa kosa gani hebu Mungu awafungue ufahamu wenu muelewe hatuonyeshi nguvu kila mtanzania anatakiwa aelewe sio ugonvi Mungu awasaidie sana katika hilo
ReplyDeleteWenyewe hawajielewi.
ReplyDeleteBakwata haitakuwa na fedha za kuendesha Mahakama za Kadhi ambazo huwa na makadhi (mahakimu) wanaohitaji mishahara kila mwezi. Serikali inapaswa kuzihudumia hizo mahakama. Mbona Serikali inahudumia Ukiristo kwa muda mrefu sasa? Serikali ikikataa kubeba hizo gharama itakuwa ni ubaguzi wa wazi na utaigharimu serikali.
ReplyDeleteJamani ni taasisi ipi ya ki kristo inahudumiwa na selikali?taasisi zote za ki kristo zilikuwa zinapata misaada kutoka nje.kwa sasa taasisi hizi zinamifuko yake ya hifadhi.selikali yetu haina dini jamani hivyo tusiibebeshe mizigo isiyokuwa yake.
ReplyDeleteAnonymous wa 8:39 AM wewe ni pimbi kabisa, tena nimeamini waislamu wote ni wapumbavu wa akili, toa mfano wa namna gani serikali nahudumia ukristu? yaani madini mengine haya ya kishetani ni hatari kabisa, wewe unafikiri hapa ni iran, ninyi waislamu huwa ni majinga sana, mmejinyanyasa wenyewe kwa muda mrefu sana kisaikolojia kwa kuendekeza mishule yenu hyo ya madrasa leo mmestuka muda umeshawatupa mkono, jitoe mianga basi kama wafanyavyo nigeria na kwingineko, shenzi taipu.
ReplyDeleteAnonymous wa 10:39, dini ya kishetani ya mamaako na babaako!toa point acha kutukana dini za watu,shenzi ww na ndugu zako midivishen five utaijua tu,paka shume wewe
Deletendio maana mnaoana makanisani..dini ya mashoga na malaya
DeleteULAANIWE KABISA WEWE,NI DINI GANI AU UKRISTU GANI UNAKUAMURU KUTUKANA DINI YA MTU?TUBU!
DeleteAnonymous wa 8:39 wewe wa hapo juu kuwa na busara na maneno unayoyatoa sio utukane watu na dini zao .weka maneno ya msingi na sio kukurupuka tu kwa jazba
ReplyDeletewewe mwenye kutukana dini za wenzio..hivi unamaana gani ..eti tumestuka muda umeisha kwisha???wewe uliyestuka zamani mbona unaelekea kiuenda wazimu..ungekuwa mwenye akili timamu usingetoa comment utumbo kama.hii..hakika sisi hatukufahamu na hatukuoni..Lakini Mola Muweza ndo Anayekuona..na kama ni kweli wewe ni mkristo safi..sasa mbona unatukana hivyo wanadamu wenziwe.?..hii unasababisha vurugu..hope unajuwa vita haina macho..na wakiamua kujiripuaa itaanzia kwako..maana wewe na wenzio kama wewe ndo chanzo cha vurugu..Acha hizo muabudu Mola wako..siku ya siku..utaMface na Atakuuliza Ulikuwa unaandika comments za namna gani?
ReplyDeleteJamani tupendane wote ni wa mungu,kwa uwezo wa kristo yesu tutashinda na kuwa wamoja.tumsifu yesu kristo
ReplyDelete