Treni Yagongwa na Gari Maeneo ya Karume Jijini Dar es Salaam

TRENI ambayo ilikuwa na kichwa kimoja ikielekea kuchukua mabehewa asubuhi ya leo imegongwa na gari kubwa la mizigo eneo la Karume jijini Dar na kusababisha foleni ndefu eneo hilo.

Tukio hilo limejiri asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi bila kufuata alama za barabarani zinazoonesha sehemu ya reli.

Akizungumza na mwandishi wetu, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed  Kanka,  alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.

Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa  Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.

Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana  na madereva wasiokuwa waangalifu.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. LICHA YA ALAMA ZA KUONYESHA KUWA ENEO HILO LINA NJIA YA RELI, NJIA ZETU ZA RELI HAZINA VIZUIZI VYA KUZUIA MAGARI AMA WAPITA NJIA PINDI TRENI INAPOPITA....

    ReplyDelete
  2. MADEREVA WA TANZANIA WAMEZIDI UZEMBE MIYE NAOMBA WAWE WANANYAMGANYA LESENI MWAKA MZIMA

    ReplyDelete
  3. YAANI MDAU NAKUPA MIA SBB KWANINI WASIEKE VIZUIZI VYA KUZUIA MAGARI AU WAPITA KWA MIGUU PINDI TRENI INAPOPITA VINASAIDIA SANA TENA SANA KUZUIA AJALI KAMA HIZI....TUNAOMBA SERIKALI IWE MAKINI KWA MIUNDOMBINU KAMA HII SBB HUKO NI KUTUUA KWA MAKUSUDI

    ReplyDelete
  4. WANYANGANYWE LESENI MADEREVA WOTE WAZEMBE KWA MWAKA MZIMA

    ReplyDelete
  5. NA KWA KAWAIDA HUWA KUNA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RELI ANASIMAMISHA MAGARI KWA TAA NYEKUNDU WAKATI WA GIZA NA BENDERA WAKATI WA MCHANA,JE HUYU MTU ALIKUWA WAPI KAMA SIO UZEMBE KATIKA KAZI?

    ReplyDelete
  6. Pale karume waliweka michuma ya kuzuia magari wakati treni ikipita, haikutumika hata siku moja wakaja weka matuta, wanapoteza pesa za umma kufanya mambo wasiyoyasimamia. Ingekuwa wameweka ile michuma chini gari ajali isingetokea. Tuwe serious kila upande, ajali haizuiwi na dereva tu, hata wao trl wangeweza kuizuia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad