Kuna barua iliyosambaa mtandaoni weekend hii inayoonekana imetoka kwenye mamlaka ya mapato nchini, TRA ikiutaka uongozi/kampuni inayosimamia kazi zake kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano kati yao kuhusiana na masuala ya promotion katika kipindi cha kuanzika mwaka 2010 – 2014.
Barua hiyo pia inaongeza kuwa:"Unatakiwa pia kuwasiliasha vielelezo vya ushahidi kuhusiana na huduma iliyofanyika na kiasi cha fedha kilicholipwa kulingana na ajira ya Abdulmalik Naseeb.”
Hata hivyo uongozi wa Diamond umedai kuwa barua hiyo nao wameiona kupitia mtandaoni lakini haijawafikia mkononi.
“Tunasikia tu kwenye mitandao hatuna taarifa nayo, maana hawajawasiliana na sisi,” amesema Salam, mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz.
“Inashangaza kuona kitu kwenye mitandao bila ya kuambiwa mhusika mkuu, tumechukulia kama changamoto zilizopo kwenye maisha,” ameongeza.
Diamond bado yupo nchini Nigeria alikoenda kutumbuiza kwenye ‘The Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2015’.
kwa uelewa wangu mdogo. hii barua ni upumbavu mtupu maana haina adress ya mwandishi wala headed paper ya tra. pia kama ni ya kweli tra wangekuwa na dispatch iliyosainiwa na aliyepokea . serikali haifanyi mambo kijingajinga namna hiyo so fikirieni namna ya kutudanganya.
ReplyDeleteTRA MMEKOSA KAZI?? DAINI KWANZA MABILIONI YA ESCORAW TUWAONE WA MAANA!!!!!!!!!!!
ReplyDeletewewe huoni kuwa hiyo ni headed paper? Au unataka uone karatasi yenye kichwa?
ReplyDeleteDIAMOND USIHOFU NI BARUA FAKE TU HIYO WANAKUONEA WIVU KWA MAFANIKIO YAKO MDOGO WANGU USIPATE PRESHA KABISA HAKUNA KITU KAMA HICHO NI VIJIBA VYA ROHO VINAWASUMBUA. SONGA MBELE USITETEREKE!!! KEEP IT UP!!!!
ReplyDelete