Je kwa nini wanawake huwa na furaha zaidi wakati wa kufunga ndoa? Hizi hapa chini ndiyo sababu

Wakatiwa kufunga ndoa wanawake wengi huonyesha furaha zao kwa namna tofauti. Wako ambao kutokana na furaha ya kuolewa wanashindwa kujizuia na kuanza kulia siyo kwa huzuni bali kwa furaha iliyopitiliza, wengine honyesha furaha zao kwa kucheza mziki kwa furaha na kumbusu mume wake wa maisha kwa mfululizo kama vile anachezea mdoli akiwa haamini kile kinachomtokea nk.

Kwa upande wa mume naye huwa na furaha kwa upande wake lakini furaha hiyo haizidi furaha ya mke, hiyo ni kwa sababu mwanaume anajua majukumu aliyojitwisha hivyo anajifariji tu kwa muda lakini anajua mziki aliouchagua utamtoa jasho

Je kwa nini wanawake huwa na furaha zaidi wakati wa kufunga ndoa? Hizi hapa chini ndiyo sababu:

1. Matatizo ya fedha yamekwisha:
Wanawake wengi wanajua kuolewa ni mwisho wa matatizo ya kifedha kwa sababu ya kile kinachoitwa mume ni kichwa cha nyumba sasa majukumu ya kujua atakula nini auatavaa nini si yake tena kuna mtu kajitwisha jukumu hilo. Kwa hiyo hata kama awe na kazi inayompa kipato cha kutosha lakini pesa yake ni yake na ya mume niya kwao. Mume hana mamlaka ya kujua kipato chake kwa sababu hakimhusu lakini yeye atakuwa anajua kipato cha mume na hata kukipangia mipango ya matumizi.

2. Kuepuka kejeli:
Wanawake wengiwanajua jinsi wanawake wenzao wanaoolewa wanavyokuwa na kejeli kwa wenzao ambaobado hawajapata wanaume wa kuwaoa, vipo vijineno neno vya kukera na kujishaua kwa wanawake wanaoolewa wakiwatambia wenzao na hali hiyo huwakwaza wenzao kiasicha kupania kwamba na wao wakiolewa watalipiza.

Lakini pia kuna kelele nyingi sana kutoka katika jamii ya kuwananga wanawake wanaokaribia miaka 30 au zaidiambao hawajaolewa. Kelele hizi huwaumiza sana wanawake ndani kwa ndani mpaka wenginehujiamulia kuzoa mwanaume yeyote atakayekuja mbele yake akiwa na nia ya kumuoa bila kumchunguza ili kuondoa kile wanachoita nuksi.

3.Kufikia matarajio yao:
Wakati wanaume wengi matarajio yao ni kujihakikishia kipato cha uhakika wakati wanawake matarajio yao makubwa ni kuolewa na mwanaume sahihi wa ndoto zake. Kuna kile wenyewe wanachoita, NDOTO IMETIMIA. Hiyo unaiona wazi kwenye nyuso zao kutokana nakupambwa na furaha isiyo kifani

4. Heshima:
Wanawake wengi huwa na furaha isiyo kifani pale wanapoolewa na wanaume wenye mafanikio, au wanaoheshimika katika jamii kutokana na nafasi zao. Wanawake huamini kwamba wataheshimika kama wenzi wao wanavyoheshimika, na hawatasita kubadili majina yao ya ubini na kujitambulisha kwa majina ya waume zao ili kuongezaheshima na kutaka kutambuliwa.

5.Gauni la harusi:
Mwanamke huvaa gauni lake la harusi mara moja tu katika uhaiwake wakati wanaume wanaweza kuendelea kuvaa suti zao za harusi wakati wowoteule wapendao. Kwa hiyo kwa wanawake jambo hilo la kuvaa gauni la harusi ndiyondoto yao na ndiyo maana wengi huzifukuzia ndoa na wanapobahatika huwa nafuraha isiyo kifani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad