Wema Sepetu hutoza mpaka dola elfu 2 kumuwekea mtu tangazo kwenye akaunti yake ya Instagram

Wema Sepetu Katika Pozi
Wakati wengine wanazitumia vibaya akaunti zao za mitandao ya kijamii kutukana na kudhalilisha watu, wapo baadhi ambao wamegundua fursa ana kuzitumia kuingiza pesa.

wema

Mtaji pekee unaohitajika ili uwe katika nafasi nzuri ya kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa na followers wengi.

Wema Sepetu ambaye ana followers 483,905 mpaka sasa kwenye akaunti yake ya Instagram amesema kuwa hivi sasa anaitumia akaunti yake kibiashara.

mi naweza kusema kwamba linapokuja swala la utangazaji (wa biashara) imerahisisha kazi Instagram sana, the more followers you got, the more money you make. So kama unataka nipost unanilipa. So imefika hivyo sababu Instagram inatumika sana kwenye matangazo sasa hivi. Mimi nimejua maduka mengine mengi labda ya nguo, accessories hata sehemu mpya za kutengeneza keki kupitia Instagram so what its matangazo.” Wema aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Ni kiasi gani Wema anatoza kuweka post ya mtu Instagram?

Tunakubaliana nikiiweka post yako ninaiacha kwa muda gani, masaa matano, naiacha siku nzima[…] awe kama na dola elfu moja flani elfu mbili hivi its okay its just a post its not like am appearing on billboard” alimaliza.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Upumbavu na uongo mtupu, kila mtu anaweza kujiwekea matangazo kwenye instagram, jaribu uone na wala sio lazima uwe na follower wengi ni bidii yako zako, kwa hiyo uongo wa wema ni upuuzi

    ReplyDelete
  2. Hahahhahaaa eti dola 2000???nayo maduka ya kina chidi mapenzi ndio walipe 2000 dollars .. Aendelee kudanganga team zake za kipumbavu

    ReplyDelete
  3. UNGEKUWA MILIONEA BASI KWA LIPI HASA MPAKA UPEWE DOLLA 2000. ACHA UONGO WEWE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad