Yanga yagomea ushindi wa Simba FIFA

Yanga jana wameliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga ushindi wa Simba walioupata dhidi yao Jumapili iliyopita wakitaka wanyang’anywe pointi tatu na kama TFF itashindwa kufanya hivyo basi wameweka wazi dhamira yao ya kulipeleka suala hilo mpaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutafuta haki yao.

Kikubwa kilichoifanya Yanga kufikia uamuzi huo na kuitaka Simba ipokonywe pointi hizo ni baada ya Simba kumchezesha mchezaji wao, Ibrahim Ajibu mwenye kadi tatu za njano.

Awali kabla ya mchezo huo, Yanga ilituma barua TFF kutaka kujua ni kanuni ipi inamruhusu mchezaji mwenye kadi tatu kuchagua mechi za kucheza wakati ipo wazi kwamba anapaswa kukosa mechi zinazofuata kisha akaendelea na nyingine, lakini ilikosa majibu na ndipo ikaamua kuandika nyingine iliyotumwa jana iliyojumuisha na azimio jingine la Simba kunyang’anywa pointi tatu.


Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alifafanua kuwa endapo kama wao wangeshinda mchezo huo basi ingebidi Simba wapigwe faini lakini kwa kuwa wameshindwa, basi inapaswa Simba wanyang’anywe pointi tatu ambapo alisisitiza kuwa katika hilo hawatarudi nyuma mpaka wapate haki yao stahiki.

“Tumeandika barua leo (jana) mapema na tayari tumeshaipeleka TFF kuhusu kutaka Simba kupokwa pointi walizozipata kwenye mchezo wetu wa Jumapili kwa kuwa walimchezesha Ibrahim Ajibu, mwenye kadi tatu za njano, kitu ambacho ni kinyume na kanuni za soka zinavyotaka.

“Na kama itatokea TFF watakosa jibu stahiki la kutupa au kushindwa ‘ku-solve’ kesi hii, basi sisi tutasonga mbele na tutakwenda Caf (Shirikisho la Soka Afrika) na kama hapo pia itakosa ufumbuzi basi tutafika mpaka Fifa, ilimradi tuhakikishe haki yetu inapatikana.

“Kama ingekuwa tumeshinda sisi siku ile, basi Simba lazima ingepigwa faini lakini kwa kuwa wao wameshinda basi adhabu yao ni kupokonywa pointi tatu, hata mechi zao walizocheza na Stand United na Prisons pia zinapaswa kupokonywa pointi kwa kuwa walikiuka kanuni kama hii.

“Kitu cha kujiuliza ni kwamba kanuni zinawezaje kubadilishwa bila ya wahusika ambao ni timu za ligi, kuwa na taarifa isipokuwa Simba pekee.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tulia mkubali matokeo asiyependa kushindwa si mshindani mjue kua simba si wajinga kumchezesha AJIBU sheria mnazozijua na wao wanazijua.yanga ondoa stress mtuwakilishe vyema leo kama taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SWALA SIO MATOKEO YA SIMBA KUMFUNGA YANGA,KINACHOSHANGAZA KWANINI HITO SHERIA WASIIJUE NA CLUB NYINGINE ISIPOKUWA SIMBA TU?MIMI HAPO NAWASIFU YANGA KWA KUTAFUTA HAKI,KAMA HAWAKUPEWA TAAFIFA YOYOTE KUHUSIANA NA MABADILIKO HAYO BASI PANGA LIPITE KWA WALIOKIUKA.

      Delete
  2. YANGA MSIKUBALI MPAKA KIELEWE HAWAWEZI KUPITINDSHA SHERIA WAKAACHWA HIVI HIVI

    ReplyDelete
  3. Ishu siyo kujua au kutokujua sheria,hapa kuna makosa yamefanyika ambayo mwisho wa siku waliohusika lazima wakubali kosa ili kutorudia tena,hata kama simba hawatanyang'anywa pointi.Kitendo kilichofanywa na bodi ya ligi kinazidi kuidumaza simba badala ya kuisaidia,kwani kila siku italazimika kubadili kanuni ili kushinda kijanjajanja tu badala ya kuwekeza kwenye kujenga timu ya ushindi.Kuifunga Yanga siyo kigezo cha ubora wa timu kwani kuna timu 14 na mechi 26ili timu iwe bingwa.Kanuni hii ni ya kurudisha nyuma nidhamu katika soka na pia ilipitishwa kijanjanja kwa manufaa ya timu fulani ambayo wanachama wake wamejaa kwenye bodi ya ligi na kamati ya utendaji ya TFF

    ReplyDelete
  4. SUALA SIO NANI KAMSHINDA NANI,AU YANGA WANAFANYA HIVYO KWA KUWA WAMEFUNGWA,UKWELI SOKA LA BONGO NI SIMBA NA YANGA,SISI AKINA COASTAL UNION NI KENGE KWENYE KUNDI LA MAMBA.KWA KUWA YANGA WAMEANZA NGOJA NA SISI TUJIPATIE KUSEMA.TFF NI SIFURI,NAHATUTAFIKA MBALI,ANGALIA JIRANI ZETU WANAVYOPOROMOKA KISOKA.

    ReplyDelete
  5. SAFI SANA YANGA,SIO KWA KUWA TFF KUMEJAA WANASIMBA BASI NDIO IENDESHWE KIWENDAWAZIMU.

    ReplyDelete

  6. Asanteni wana Yanga kwa kuliona hilo.
    kulikuwa na makosa mengi mechi ya prison na simba,ila kwa kuwa
    hata yangesemwa yasingesikika kama nyinyi wanayanga ambavyo mmeanza.

    ReplyDelete
  7. Uchungu tu wa kufungwa hamna lolote! hata kama asingecheza yeye angecheza mwingine tena siajabu kichapo kingekuwa kikali zaid! Na hao TFF walishasema kuwa kwa mujibu wa kanuni mpya timu inaweza kuchagua mechi za kukaa nje! nendeni hadi akhera ila hakatwi mtu point na poleni kwa kipigo!

    ReplyDelete
  8. Sasa Simba ikatwe points kwa kosa lipi ninyi wateja(yanga) wa Simba? Iwe Kanuni zimetolewa kwa kuficho au katka mkutano wa hadhara, ukweli unabaki kuwa kanuni zipo na hata ninyi hamkanushi kuwepo kwa kanuni hizo. Hivyo simba hawajakiuka kanuni yoyote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad