Kuhusu Zitto Kabwe: CCM wamecheza game of mind kuelekea uchaguzi mkuu

Zitto Kabwe
Maoni Huru kutoka kwa Mdau:
'Hatujui kweli kinachofurukuta mdani ya CHADEMA na hatujui kama kosa lilikuwa linavumilika ama haivumiliki.

Ila kitendo cha mahakama kufuta kesi ya Zitto haraka haraka inaweza ikawa ni game mind ya kisiasa ya CCM kwa sababu wanajua kuwa wazee wa kukurupuka watamfukuza haraka haraka na lazima kuna damage itatokea.

Au mnadhani kwa nini kesi imefutwa kuelekea uchaguzi? 

Mimi sio mamluki hata huyo ZZK, sijawahi kumuona zaidi ya kwenye magazeti, ila kilichopo kwa sasa ni kuwa CCM imechokwa na CHADEMA haijajiandaa'

By Saint Ivuga

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo jaji aliyefuta kesi atakua kapewa rushwa

    ReplyDelete
  2. Hahahahahaha! una maakili mpaka basi.

    ReplyDelete
  3. CCM IMECHOKWA NA CHADEMA IPO BOMBA HAKUNA KULINDANA KAMA CCM WANAVYOLINDANA. PEOPLES POWER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. MI NAKIPENDA SANA CHAMA CHA CHADEMA NA NDO CHAMA CHANGU ILA DU! SOME TYME HUWA WANAKURUPUKA SANA, WAO WANAONA KAMA WANAMKOMOA ZITO ILA HAWAJUI THAMANI YA ZITO WANAAMUA KUCHUKUA HATUA BILA KUTAFAKARI NA CCM WANAPATA LAKUONGEA. MIE NITAMFATA ZITO ATAKAPOKUWA NO MATTER WHAT

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chadema ilitokea kupendwa na wengi,hasa wapenda haki,
      lakini kwa sasa inapoteza mwelekeo.

      Delete
  5. CHAMA LAZIMA KIWE NA MAAMUZI MAGUMU SIO KULINDANA LINDANA TU WATU WANAKULA NCHI MABILIONI WANASEMA VIJICENT SASA HELA NI MATIRION?? MILIONI 10 ZA MBOGA JE ZA MCHELE ZITAKUWA NGAPI???WATANZANIA LAZIMA TUBADILIKE

    ReplyDelete
  6. Jamani katiba ya chama inasema kwamba mtu yeyote anayepeleka mambo ya chama mahakamani inatakiwa afukuzwe na yeye zito alikuwa analitambua hilo. Me kwa uelewa wangu naona chama kipo sahihi. Kwa sababu yeye Zitto alipoona yametikea yale ilitakiwa azungumze vizuri na viongozi wake ikiwezekana kuwaomba msamaha, sasa toka mwaka jana mpaka leo ameshindwa kujishusha na kuyamaliza na viongozi wake, Na cku zote Watanzania tunalalamika kwamba sheria zinavunjwa hivyo CHADEMA ni mfano wa kuigwa kwamba sheria ikitungwa hakuna wa kuivunja hata uwe na ushawishi kiasi gani.

    ReplyDelete
  7. eenhe mdau nakuunga mkono asilimia 99...

    ReplyDelete
  8. MINE IS LOADING WADAU

    ReplyDelete
  9. Kwani Zitto anadai ninj ndani ya CDM?Tufahamu anachodai ZZK hadi akaenda Mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama ndio tuje hapa kutokwa povu.

    ReplyDelete
  10. Ni kweli ccm walikuwa na mpango wa kumtumia zzk,lakini baada ya kuibuka UKAWA na kuwa tishio,ccm imemtema mazima na sasa imemchinjia zzk baharini.

    ReplyDelete
  11. Sheria ifate mkondo

    ReplyDelete
  12. KATIBA IMECHUKUA MKONDO WAKE!!!!

    ReplyDelete
  13. Katiba ya chama inakiuka haki za binadamu. Kwa nini imkataze mwanachama kwenda mahakamani ilihari mtu anaona kabisa kwamba haki yake itanyongwa ndani ya chama! Hakuna demokrasia ya kweli hapo!

    ReplyDelete
  14. Sasa Chadema wasingefata katiba inavyotaka ingetokea baadae mwanachama mwingine akapata ishu kama hiyo wangefanyaje? Sheria ni msumeno haitakiwi kupindishwa bila kujali nani wala nani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad