CCM wamsimamishe Zitto Kabwe Kugombea Uraisi 2015

Wadau, tangu Zito Kabwe aingie kwenye mgogoro wa kimaadili na kilichokuwa chama chake cha awali CHADEMA, umaarufu na kukubalika kwake katika chama tawala ccm kumeongezeka sana. Tumeona viongozi wa ccm wa kitaifa hadi waandishi wa mitandaoni, wakimpigia debe sana Zito kwamba ni kijana shupavu; mchapa kazi; mzalendo; na kiongozi bora asiyestahili kuwa chini ya uongozi wa mtu mwingine yeyote. Tumemsikia Nchemba akimsifia sana ZITO kwamba ni mtu ambaye hakuwa kiwango cha CHADEMA. Wengine wanasema bila Zito CHADEMA hakipo n.k.


Baada ya Zito kufukuzwa CHADEMA, ccm wameumia sana kwamba sasa. Ccm wamekuwa wakilia sana kwamba CHADEMA kimekufa kwa kuondokewa na huyu mtu Zito ambaye mara zote ccm wamekuwa wakimpgia CHAPUO LA wazi kwamba anastahili kuwa Mwenyekti wa taifa na mgombea wa uraisi kwa kuwa anasifa zote.

Sasa sina shaka, kwamba CCM ina uhaba wa watu wenye sifa za kugombea uraisi hadi wanaanza kuambizana wasinyosheane vidole maana wote ni wachafu;, na hivo kuanza sera mpya ya kutafuta aliye msafi angalau kuliko wenzake. Sera ya kutafuta kisafi katika jalala.

Ninaomba ccm msihangaike tena kutafuta mtu msafi jalalani. Zito Kabwe yupo huru hana chama ni mnampenda, mnamkubali kwa sauti moja na kwa mujibu wenu anasifa zote pasipo swali. Mmvalishe jembe na nyundo, mmfanye mwenyekiti wenu wa taifa na mgombea wa kiti cha Uraisi ili mshinde. Hapo mtapiga bao la kisigino kwa sababu mtakuwa mmesimamisha mgombea ambaye anauwezo kuliko ccm wote, na pili vyama vya upinzani vitakuwa vimekufa kwa kuondokewa na Zito.

Sina wivu na ccm, ninawatakieni mema. Au mnasemaje wadau?

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kiongozi mzuri bali siyo kwa nafasi ya Urais

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad