Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo March 14 ametoa gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi wake atatoa gari hiyo.
Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.
Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.
Je Unafikiri Kufukuzwa Chadema Kumemuongezea Umaarufu Ama la?
Zitto tupo na wewe bega kwa bega popote uendapo
ReplyDeleteHATA CHENGE NA TIBAIJUKA PIA WALIPOKEWA KWA SHANGWE PIA
ReplyDeleteWAAAMBIE HAWA!!!
DeleteWao walitoa nini katika jamiii
ReplyDeleteni huko kigoma tu ndio wanaomuona kwani huko bado kiza
ReplyDelete