Afrika Kusini hakukaliki, raia wa kigeni washambuliwa, baadhi wauawa, Malawi kuwaondoa watu wake

Vurugu kubwa zilizoenda sambamba na uporaji mali, zimeibuka jana usiku kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambapo raia wa kigeni wamelengwa.

Baadhi ya watu wameuawa na maelfu kukimbia makazi yao kufuatia kuendelea kwa mashambulio hayo.

Makundi makubwa ya raia wa Afrika Kusini yalikuwa yakizunguka kwenye maduka mbalimbali yanayomilikiwa na wageni na kupora mali. Fujo hizo zinaendelea katika maeneo mbalimbali ya Durban.

Maduka mengi yamechomwa moto licha ya polisi kuongeza nguvu ya ulinzi.

Mwamvita Makamba ni miongoni mwa raia wa kigeni walioathirika na fujo hizo ambapo gari yake ilipigwa risasi.

Wakati huo serikali ya Malawi jana ilisema kuwa itawasaidia raia wake kuondoka nchini humo. Zaidi ya raia 360 wa Malawi wamepoteza makazi yao na kila kitu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad