HATUA ya mawakili wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kutengeneza ubishi wa kisheria katika agizo la Polisi la kuwasilisha nyaraka za mali za Askofu huyo, imeelezwa kuwa ni ukaidi ambao hautamsaidia kisheria.
Badala yake, kwa hatua hiyo ya mawakili hao, Jeshi la Polisi limewekewa mazingira mazuri ya kuchukua hatua ya pili ya matumizi ya nguvu katika kutekeleza agizo lao, baada ya hatua ya hiyari kushindikana.
Wakizungumza na gazeti hili jana, wanasheria mbalimbali walishangazwa na ubishi wa juzi, uliotokana na barua ya mawakili wa Askofu Gwajima kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Katika barua hiyo, mawakili hao walitaka Polisi itoe agizo la maandishi la kuwasilisha nyaraka hizo, litakaloeleza vifungu vya sheria vinavyomtaka mteja wao kuwasilisha nyaraka hizo.
Ukaidi wa Gwajima
Barua hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala, iliwasilishwa juzi mchana katika jeshi hilo ikiwa ni siku moja baada ya Askofu Gwajima kutakiwa kuwasilisha nyaraka 10 zinazohusu umiliki wa mali zake, Aprili 16 mwaka huu watakapoendelea na mahojiano.
Mawakili hao kwa niaba ya mteja wao wameliomba Jeshi la Polisi kumwandikia barua rasmi Gwajima, wakiainisha nyaraka wanazozihitaji, pamoja na vifungu vya sheria vinavyotumiwa na jeshi hilo kutaka nyaraka hizo.
Mawakili hao wanasema watashukuru kupata hati hiyo ambayo wamedai hawaijui jina, lakini wanaamini Jeshi la Polisi litafahamu jina la kisheria la nyaraka husika inayotumika kumtaka Gwajima, awasilishe nyaraka wanazozihitaji.
Aidha wanasema askofu Gwajima atakapopata nyaraka anayoihitaji, atatimiza mwito na kuchukua hatua stahiki za kisheria.
Nyaraka 10
Nyaraka hizo ni Hati ya Usajili wa Kanisa, Namba ya Usajili, majina ya Baraza la Wadhamini (Baraza la Kiroho), idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia, nyaraka za helikopta ya Kanisa na muundo wa uongozi wa Kanisa.
Nyingine ni Waraka wa Maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za Kanisa na nyaraka zinazoonesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari. Pia waliagizwa kufuatana na mtu anayepiga picha za video kanisani hapo.
Ushauri
Wakifafanua kuhusu ubishi huo wa kutaka sheria inayotumiwa na Polisi kuagiza nyaraka hizo, wanasheria waliozungumza na gazeti hili walisema hakuna sheria yoyote inayomzuia Polisi kudai umiliki halali wa mali au nyaraka endapo watazihitaji.
Mwanasheria Dk Damas Ndumbaro, alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai na ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, askari Polisi amepewa fursa ya kufanya ukaguzi wa mali na nyaraka zozote bila ya kuzuiwa na mtu.
‘’Polisi anaweza kufanya ukaguzi nyumbani kwako bila kuwa na hati ya ukaguzi na anaweza kuwa nayo. Lengo lao ni kukamilisha masuala yao ya kipolisi tu,’’ alisema mwanasheria huyo.
Askofu Gwajima ajipalia makaa...Hatua ya MAWAKILI wake Kutengeneza UBISHI wa Kisheria Katika Agizo la Polisi Utamzidishia Matatizo
7
April 12, 2015
Tags
anachosema mwanasheria Dk Damas Ndumbaro ni sawa, lakini JE? nyaraka hizo zinahusikaje na shauli la kukashfu na kutukana. Au kuna shauli jingine, lakini kwa nini sasa? Hizo mali zipo siku nyingi. Endapo umiliki wa helikopta si halali, polisi (serikali) ilaumiwe kwa UZEMBE? Ujio wa helikota hiyo uliwekwa hadharani, polisi hawakuona haja kujiridhisha? Kama kuna jambo la kiharifu Gwajima anahusika waseme ili sisi wenye nchi tujue. Kutosema kweli kunaleta hisia labda ndiyo ule mchezo wao wa kubambikiza watu kesi, itazidisha chuki dhidi ya polisi. … WASEME UKWELI; kama Gwajima zungu la unga ama ni urais au vinginevyo. Wafanye kazi kisheria na si kuburuzwa tu….
ReplyDeletePolisi hana muda maalum wa kazi.inasemekana ameingiza vtu vingi bila ushuru kwa kivuli cha kanisa yet ni chake binafsi.
Delete@11;22, Wewe unaongea kiushabiki hujui sheria..huyu mchungaji kaingia mwenyewe mtegoni na mali alizonazo si halali na kama zingekuwa halali basi asingeweza kuweka pingamizi kutumia mawakili wake.. huyu ni mwizi kama wezi wengine ,, ashughulikiwe ipasavyo
ReplyDeleteyaani huu ni upuuzi. sasa unamwita mtu kwa kosa linguine halafu unaanza kuuliza maswali tofauti? kweli hilo linatokea kwetu Afrika tu na wala si kweingineko. Yaani inaonekana kabisa sasa ni visa na sio kazi tena
ReplyDeleteHali ilivyo hivi sasa katika jeshi la police nmbaya mno. Raia hawana imani hata kidogo na jeshi hilo. Hiyo sheria ya kuwaruhusu wao kukagua bika hati ya ukaguzi ni kandamizi. Hapo ndipo utasikia mtu kawekewa silaha ya kivita na hao hao askari ktk eneo la ukaguzi. Km mtu anakamatwa akicheza mchezo wa pool table then akifika kituoni kesi inakuw a ni ya kukamatwa na bangi na madawa ya kulevya je inakuwaje kwa suala kubwa. Sasa nyie viongozi wa jeshi hilo endeleeni tu kuzunguka kwenye viti maofisini huyo mkisubiri taarifa kwa wa chini yenu. Hali mbaya huku mtaani.
ReplyDeletewewe @ 2:21 na huyo mwanasheri sijui DK nani sijui na hao polisi wenu ndiyo hamjui sheria kabisaa au mnadhani sheria ni siasa, hakuna chombo chochote kilicho juu ya sheria, polisi pia wanaongozwa na sheria. Gwajima kamwibia nani?
ReplyDeleteNa akome eeee ee kama alivyo mwambie pengo
ReplyDelete