Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.
Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!
Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.
Si kipaumbele chake akiwa bugeni suala analohangakia ni kuwashughulikia mafisadi
ReplyDeleteSasa anataka halima akajenge mwenyewe, jukumu lake ni kuishinikiza serikali ...
ReplyDeletesasa kama jukumu lake ni kuishinikiza serikali mbona haishinikizi miaka yote aliyokaa bungeni???..kamejaa umbea tu
ReplyDeleteTujaribu kuwa na hekima katika kufiria mambo kwa kina, Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania chama kilichoko madarakani ndicho sera zake hutekelezwa na serikali. Nendeni mkaangalia kama hiyo barabara ipo ktk sera ya chama kinacho ongoza nchi ndiyo useme
ReplyDeleteMBONA BARABARA NYINGI TU ZILIAHIDIWA KUJENGA HATA KWA KIWANGO CHA VUMBI TU HAZIJAJENGWA!!! SEMBUSE HIYO YA MADALE TENA KIWANGO CHA LAMI.??? HALIMA WEE JEMBE USIVUNJEKE MOYO TUPO BEGA KWA BEGA NA WEWE!!! YEYE KAONA HILO LA BARABARA NI MANGAPI UMEFANYA HAYO HAYAONI??
ReplyDeletehili domo linaipigia kampeni ccm za chini chini. akajenge yeye sasa si anahela za cmm!
ReplyDeleteApambane na mawaziri halafu waziri huyo huyo akaipangie bajeti barabara ya jimbo lake....thubutu!!
ReplyDelete