'Hatuko Tayari Kuzibwa Midomo Tunamtaka Lowassa Agombee Urais 2015' Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Jijini Mwanza

Shinikizo la kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuchukua fomu ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu, limeendelea na safari hii wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya jijini Mwanza, wametoa tamko la kumtaka kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, viongozi wa vyuo vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi  na Tiba za Afya (CUHAS), walimtaka Lowassa kuchukua fomu ya kuwania urais wakati ukifika.

Viongozi hao waliyazungumza hayo wakati wakikabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo Daima, jijini Mwanza.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa CUHAS, Godfrey Kisigo, alisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anapendwa na kila Mtanzania.

 Alisema wanamuomba muda ukifika awe mtu wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi ya urais.

Tamko hili ni la vyuo  vikuu vyote vya Mwanza, sauti zetu ni za busara kwa sababu zinataka kuikomboa nchi yetu kwa miaka 10 ijayo, tunayo imani kubwa na Lowassa katika hatma ya nchi hususan elimu kwa watu wote,” alisema na kuongeza:

Hatma ya nchi hii ipo mikononi mwako na sisi wanavyuo hatuwezi kusubiri kuona tunakosa kiongozi atakayelisaidia Taifa kwa kuzibwa midomo, tupo tayari kufa ili uwe rais uokoe watakaobaki na Tanzania.”

Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi SAUT, Christopher Mkodo, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisijaribu kukata jina la Lowassa kwani Tanzania bila kiongozi huyo Watanzania watakuwa wamenyimwa fursa ya kupata maendeleo ndani ya miaka 10.

Waliitaka CCM kusikiliza maoni ya wanachama wake  vinginevyo chama kitaharibika.

Mwakilishi wa CBE, Paul Dotto, alisema Lowassa ni chaguo la wanafunzi wa vyuo vikuu na wana imani ataifikisha Tanzania katika uchumi wa kati kabla ya malengo yaliyowekwa na Serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad