Jack Dustan: Sisi Mastaa wa Kike Ndio Vinara wa Kuchukua Waume za Watu Bongo Tusipobadilika Watatuua

Staa aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan amefunguka kuwa mastaa wamepachikwa nembo ya kuwa ni vinara wa kubeba waume za watu jambo ambalo linawapa sifa mbaya.

Akizungumzia mwenendo wa mastaa wengi kuhusishwa na skendo ya kutembea na waume za watu, Jack alisema:

Yaani sisi mastaa tumepachikwa nembo ya kupora waume za watu. Imefika wakati hata kama umempata mpenzi wako mtu anakuuliza umempora nani. Huwa inaniuma sana.

Kimsingi tuna sifa mbaya na tusipobadilika waume za watu hawa watatuua.”

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad