Jakaya Kikwete Ajipalilia na Kujivunia Miaka Kumi ya Kuiongoza Tanzania kwa Mafanikio Makubwa

SERIKALI ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Aidha, Rais Jakaya Kikwete anayeiongoza awamu hiyo, amesema anatumaini uchaguzi mkuu ujao utakaotoa wabunge, madiwani na rais ya awamu ya tano unaotarajiwa kufanyika Oktoba , utakuwa huru na wa amani.

Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi urais mrithi wangu katika hali ya utulivu,” Rais alisema.

Rais aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson.

Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia,” Rais Kikwete alisema na kuongeza anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo mwaka 2020.

Je kwa Upande wako unaona JK ameleta Mafanikio Tanzania ?

Udaku Specially Blog

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wizi mwingi wa mali za umma na rushwa kukithiri isivyo kawaida

    ReplyDelete
  2. YEYE AKIWA MMOJA WAPO!!!

    ReplyDelete
  3. Kuzidi kupolomoka kwa Elimu. Huduma za afya. Yaani nchi imezidi kuyumba katika nyanja muhimu na muhimu. Madawa hakuna. Wizi kila kona na ufisadi uriokithiri. Nchi hata hajielewi.

    ReplyDelete
  4. Rais ajae hasipafanye ikulu kua pango la waranguzi kama huyu anaemaliza, tukimbaini tutaweka kwa nguvu

    ReplyDelete
  5. Hii inashangaza sana,Hiv Mheshimiwa hujui kama kuna marehemu wana pokea mshahara mpaka leo?mbaya zaidi wezi wenyewe wapo na wanajulikana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad