Staa mrembo wa Bongo Movies, Mariam Jolwa ‘Jini Kabula’ amesema kuwa anguko la soko la filamu za Bongo asitafutwe mchawi, kwani wasanii wengi wanaigiza chini ya kiwango na ndiyo maana kazi zao hazifanyi vizuri, licha ya kutumia gharama kubwa kuziandaa.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Dar es Salaam jana, Jini Kabula alisema kuwa ni filamu chache zinazofanya vizuri sokoni, ikiwemo ya Chozi la Wanjaa iliyochezwa na Aunt Ezekiel, Kulwa Kikumbi ‘Dude’ na wasanii wengine ambazo zinaonekana kuwafurahisha watu, isipokuwa nyingi zinatengenezwa kwa kulipuliwa.
“Hakuna haja ya kumtafuta mchawi wa anguko la filamu nchini, kwani wengi wanatengeneza kwa kulipua, endapo waandaaji wasipobadilika, fani hii itakuwa haina maana tena kwa waigizaji,” alisema.
Jini Kabula Ataja Mchawi wa Soko la Filamu
1
April 29, 2015
Tags
Ni kweli kabisa, pia wasanii wengi wa bongo muvi hawana mwelekeo zaidi ya kujitanua kwenye mitandao ya kijamiii
ReplyDelete