Lulu: Kuharibu ni Rahisi Kuliko Kujenga 'Habari za Ubaya Zinasambaa Sana Kuliko za Kujenga'

Staa wa Bongo Movies,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ anasema baadhi ya watanzania wanapoteza muda wao katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwaumiza wengine na kuwatusi bila sababu, huku wakiwa makini kusikiliza mabaya na kuyavumisha tofauti na taarifa njema zenye faraja kwa jamii.

Ukiwa kama Binadamu kila jambo ukitaka kulisambaza kwanza tafakari katika nafsi yako, je huyo unayemtenda hana maumivu kama mwanadamu, tumekuwa mabingwa wa kuwaumiza wengine kupitia mitandao ya kijamii bila huruma,”

Sijui kuna mtu anayeombea maumivu kila mara kwani iwe Lulu kila jambo baya, na asiwe mtu mwingine hiyo inaonyesha hata wanaojiita marafiki zangu waweza kuwa maadui zangu,”anasema Lulu.

Lulu anasema kuwa kuharibu ni rahisi sana kuliko kujenga kwani mara nyingi habari za kujenga ubaya zinasambaa sana kuliko wema, lakini anaamini kuwa Mungu ndio kila kitu na ajua ukweli wa kila jambo na hawezi kumhukumu mtu yoyote.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acha ujinga na kujiongelesha kama mjinga ile picha na marehemu ilikuwaje

    ReplyDelete
  2. JARIBU KUJIWEKA MBALI NA MITANDAO UTAFANIKIWA HIYO MAMBO YA KUJISHEBEDUA MITANDAONI ITAKUMALIZA. BORA KUJIEPUSHA NA HILO JINAMIZI BADO LINAKUZUNGUKA NA MUOMBE SANA MUNGU WAKO

    ReplyDelete
  3. Hivi Lulu hujui malipo ni hapa hapa duniani? wewe ulivyojibebesha mme wa mtu na kuanza kuhangaika naye waganga na kila aina hukujui huwa yana mwisho? pole umri na mambo yako ni vitu viwili tofauti kabisa khaaa sasa ukifikisha miaka 30 itakuwa je? si utaandikwa kwenye kitabu cha Guinness.... shame on you hata ningekuwa ndugu yako hakika nisingethubutu kusema your my relative phuuu

    ReplyDelete
  4. Ulizidi sana kujitangaza kwenye mitandao, kujionyesha na kujivuna na ustaa wako na kujisahahu kama unabiriwa na kesi ya mauaji... ingawa uliachiliwa huru utajipa kifungo cha ndani wewe mwenyewe. Binaadamu wataendelea kukuhukumu, jambo hilo huwezikulizuia. Ulitakiwa kukaa kimya kujiweka mbali na mitandao ya kijamii kwani ulijisahahu sana....Pole sana binti kwa yanayokukuta

    ReplyDelete
  5. Anae hukumu ni mungu pekee nasio binadam hivyo basi mabaya ya lulu na mazuri ya lulu ni mungu pekee ndio anayejua, huenda wanao mtuhum huyu mtoto ndio wanahukum kubwa kwa mungu kuliko wanavyofikilia, mwacheni mtoto wawatu aendelee na masomo yake (hakuna aliye mkamilifu hapa duniani).

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad