Magaidi Wavamia Chuo Kikuu Cha Garrisa Kenya......Waliofariki mpaka sasa ni 15

Takriban watu 15 wameuawa baada ya watu watano wanaodaiwa kufinika nyuso zao kushambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.

Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.

Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.

Taarifa  zaidi  zinaarifu  kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.

Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.Wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.

Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.

Wanafunzi 27 wamefanikiwa kutoroka na sasa wako katika kituo kimoja cha kijeshi.

Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulizi hilo ijapokuwa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab limeshukiwa kutekeleza shambulizi hilo.

Chuo hicho ndio taasisi ya kipekee ya masomo ya juu katika eneo hilo kilichofunguliwa mwaka 2011 na kiko takriban kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dini ya amani,magaidi walikuwa wanauliza wanafunzi maswali yanahusu quruan ukishindwa kujibu unauliwa.

    ReplyDelete
  2. Mimi nasikia kitabu kitakatifu cha dini ya kiislamu kinafundisha kilipiza kisasi je nina kweli,naomba mtujuze.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ha ha ha siri ziko nyingi cha maana ni kumwomba Mungu awangaamize mabedui

      Delete
  3. KULIPIZA KISASI INARUHUSIWA NA INA SHERIA ZAKE.HAWA AL SHABAB SIO WAISLAM, COZ UISLAM HAUTUFUNDISHI HAYO WANAYOYAFANYA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad