Mama Lulu Michael Afunguka Kwa Uchungu 'Mwanangu Yupo Katika Wakati Mgumu Sana Mwacheni Mwanangu Apumzike'

Na Imelda Mtema
Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!

YOTE HAYA KISA MITANDAO
Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.

TUJIUNGE NA MAMA LULU
Akizungumza na gazeti hili, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.

MANENO KUNTU
“Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi.
“Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia.“Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?
“Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue,” alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Mzazi huyo aliendelea kusema kuwa, anaamini kwamba mambo mengine yanayotokea katika maisha ya mwanaye ni mipango ya Mwenyezi Mungu hivyo haoni sababu ya Lulu kubebeshwa lawama za ajabu.
Mama huyo alisema kuwa watu hao wanataka mwanaye afe kwa sababu kuna wakati anakosa raha ya dunia hivyo naye anatamani afe tu ili watu wamwache apumzike.

KIPINDI KIGUMU CHA MITIHANI
Mama Lulu aliendelea kueleza kuwa, Lulu kwa sasa yupo kwenye kipindi kigumu cha mitihani (anasoma Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Magogoni-Posta jijini Dar) lakini anawezaje kufanya vizuri huku kuna baadhi ya watu wakimsemea maneno yasiyofaa?!“Atawezaje kufanya vizuri wakati watu wanamwandama kila kukicha? Huko kote ni kumkatisha tamaa hivyo nimemwambia mwanangu amwachie Mungu na kusali sana,” alimalizia mama Lulu.

HUYU  HAPA LULU
Baada ya kuzungumza na mama huyo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu ili kumsikia na yeye ana mtazamo gani kuhusu shutuma hizo ambapo alisema kila kitu anamuachia Mungu pekee na si mwingine hivyo kwa sasa aachwe asome.“Kila kitu changu nimemuachia Mungu maana hakuna mtetezi wangu zaidi yake, ndiyo maana ninasali sana ili Mungu anisaidie,” alisema Lulu.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mh! huyu binti akafanyiwe sala ya toba na ukombozi si bure maajenti ya kuzimu yatakuwa yamemvaa bila yeye kujua hilo ndilo suluhisho.

    ReplyDelete
  2. Wewe mama Lulu tena hata wewe nakushamgaa unahongwa nyumba na mwanao unaipokea bila kujiuliza alikuwa jela ametoka juzi kapata wapi hela mpk kununua kujenga.... sio neno ndio maisha mwanao aliochagua kuishi soo mwache alinywe kabisaa!!!
    Anasoma................... ajithidi sana maisha sio lelemama

    ReplyDelete
  3. tatizo lulu mdogo sana......na analala na mibaba mikubwa mno.hata mimi sikuwahi kulala na mijitu mizima nikiwa na umri mdogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hivo waataka Lulu awe kama wewe kama nani wako hasa?Kumbuka wewe si lulu.

      Delete
  4. Wewe mama ulitakiwa ukae kimya,, unalialia hujui mambo ya walimwengu? watasema tu hata akifa,binaadamu watasema hawaangalii wema wake kwani hakuna jema alilotenda,,kwa hiyo mkae kimya muangalie dunia inavyokwenda

    ReplyDelete
  5. Nimekuonea huruma mama,Kabla ya kumuachia Mungu muombee mwanao pepo la umalaya limtoke.Tutaacha kumsakama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msakamen ila wajua ya leo kesho haujui watoto wako pia watakaa vip yaeza kuwa zaidi

      Delete
  6. lulu acha umalaya nikikukamata na mumewangu nakata hiyo shingo mfyuuu

    ReplyDelete
  7. Huyu mama nae inaezekana ni malaya km mwanae kwani naamini tunda huangukia karibu na mti. Asituchoshe na machoz yake ya kinafiki ulivokua unantuma kwa mabwana wa watu hukujua mwisho wake upo. Thats what she deserve. Mxchwiiiii

    ReplyDelete
  8. ww mm lulu kweli unaumia ila makosa ni yako ,unamponza mwanaona mtoto mdg mmbo yake makubwa kukupita ww mmaake uliemzaa ,akulishe ,akuvishe,yy kawa mzazi ww umekua mtoto kiac huwrzi kusema chochote juu yake c anakuhumia yy ndio jembe lako ss hayo yanamkuta sababu ya tamaa kulala na waume za watu ili akiz i majukum alokua nayo yakulea family ..ila kaa ukijua ngoma ikivumaa sana haikawii kupasuka ..fanya ibada umuombeee mwanao pepo la ngono limtoke

    ReplyDelete
  9. mama mwenyewe changudoa,, anafirisha ile mbaya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad