Mawakili wa Gwajima Wajibu Mapigo Waiandikia Barua Polisi Kuhusu Uhalali wa Kumtaka Gwajima Awasilishe Nyaraka 10 za Mali Zake

Mawakili wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, wameandika barua kuliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuandika kimaandishi nyaraka wanazozihitaji azipeleke pamoja na vifungu vya sheria vinavyomtaka awasilishe nyaraka hizo.

Barua hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala iliwasilishwa jana mchana katika jeshi hilo, ikiwa ni siku moja baada ya jeshi hilo kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka 10, Aprili 16 mwaka huu watakapoendelea na mahojiano.

Gwajima aliitwa kuhojiwa na jeshi hilo mara mbili kutokana na kufunguliwa jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Katika barua hiyo, mawakili hao kwa niaba ya mteja wao wanaliomba jeshi la polisi kumwandikia barua rasmi kimaandishi, Gwajima wakiainisha nyaraka wanazozihitaji pamoja na vifungu vya sheria vinavyotumika na jeshi hilo kutaka nyaraka hizo.

Mawakili hao wanasema watashukuru kupata hati hiyo ambayo hawaijui jina lakini wanaamini jeshi la polisi litafahamu jina la kisheria la nyaraka husika inayotumika kumtaka Gwajima awasilishe nyaraka wanazozihitaji.

Aidha wanasema Askofu Gwajima atakapopata nyaraka anayoihitaji atatimiza wito na kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Magaidi hawawaoni wanaopora silaha vituoni mwao wanaleta wivu ktk mali za watu kwasababu wao hawana uwezo wa kuvipata.,ngija mvamiwe vyumbani kwenu su mnajiona mpo pekeenu duniani hayaaa.,jana mgimo tu wa madereva wamerukaruka wewe wakaona pointi zao bata.,lindeni mikusanyiko ya raia acheni kutaka kujua mtu alipata vp kitanda au kochi analokalia matope tu hayo....,

    ReplyDelete
  2. hapo inaonyesha wazi ni jinsi gani polisi wetu wamekosa weledi katika utendaji wao.Wanasukumwa tu na wanasiasa. Wakiambiwa PIGA, UA, PORA wanajifanyia tu hata kama hawatakuwa na majibu sahihi watakapoulizwa.

    ReplyDelete
  3. Movie imefika patam sana. Polisi watu shule ndogo hata sheria hawajui maskini. Waliwahi nikamata na gari ya wizi wa gari langu wenyewe ambalo hata TRA inaonesha ni la halali. Tulipokataa kutoa hongo na kukomaa hio kesi iliishia ofcn mwao ingawa walinisumbua mnoo. I hate those policemen hawana utu kabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad