Habari zaidi kutoka kwa aliyekuwa rafiki wa karibu wa Rehema nchini China, (jina lake linahifadhiwa) zinasema kuwa wamekuwa wakihangaika ili kupata fedha za kusafirisha mwili huo lakini imekuwa ngumu kupatikana.
Chanzo hicho kilisema kuwa kimefanya mawasiliano na baadhi ya ndugu wa marehemu ambao nao wanajikusanya kwa ajili ya kupata fedha hizo ili kuurudisha mwili nyumbani Dar kwa mazishi.
“Yaani huku tunapata tabu sana na tuna uchungu kwa kuwa fedha zilikuwa zikihitajika nyingi sana lakini tunashukuru taratibu zinaenda sawa karibu tutaleta mwili nyumbani,” alisema rafiki huyo.
Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa kifo cha ndugu yao ni pigo kubwa ukizingatia amefia ughaibuni na fedha za kumleta zinahitajika nyingi hivyo wamekaa na kumuomba Mungu ili mwili ufike Bongo waupumzishe.
“Msiba wa mdogo wetu umetupa wakati mgumu sana jamani, ukizingatia amefia mbali sana na kumleta huku ni fedha nyingi mno, hivyo tunamuomba Mungu tu ili mwili ufike na tuupumzishe katika makaburi ya nyumbani,” alisema ndugu huyo.
Toa Maoni Yako Hapa Chini
Sijaona mashiko ya habari hii!!!!!mtu yoyote akifa ndugu na marafiki lazima wawe na uchungu,au ukosefu wa fedha ya kusafirisha mwili ndio habari?wekeni habari zenye kueleweka
ReplyDeleteinnalillah wainna ilayhi raj..uuun
ReplyDeleteAlienda kufanya shughuli gani huko maana watu wanaenda huko but hawana cha maana kilichowapeleka.
ReplyDeleteanyway poleni wafiwa
Alienda huko kufanya shughuli gani?maana wabongo tunakimbilia nje bila shughuli maalumu zaidi tu ya kuuza sura.
ReplyDeleteanyway poleni wafiwa
Tatizo wabongo wengi tunapenda kukimbilia nje hata kama hatuna shughuli ya maana ya kutupeleka huko.Yanapotokea matatizo kama haya watu wanaanza kuhaha kusafirisha mwili.,poleni wafiwa
ReplyDelete