Nashangazwa na Msimamo wa Mbowe Kuhusu UKAWA - Zitto

Katika gazeti la changamoto katika ukurasa wake wa kwanza unasomeka "Zitto azidi kuwaumiza CHADEMA" na habari hiyo ukiifuatilia ndani inaeleza kuhusu kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe na jinsi Zitto alivyoipokea.

Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba, Zitto hakutarajia mtu ambae yeye anamuheshimu katika siasa kuwa na misimamo isiyo tanguliza maslahi ya taifa mbele na badala yake kushikilia matatizo yao yaliyojitokeza huko nyuma ambayo kimsingi yalihusu nafasi za kiuongozi.

Zitto alieleza kuwa kwa sasa hayupo tayari kujibizana na viongozi tena kwa kuwa amekuwa akisema hivyo kila mahali anapokwenda kufanya mikutano yake na amewekeza nguvu nyingi katika kukitangaza chama chake kipya. Pamoja na malengo hayo, ila kwa kauli ile ya jana ameona hana budi kuitolea maelezo!

Zitto alisisitiza kuwa matatizo yake binafsi na viongozi wa chama chake cha zamani yasipewe kipaumbele kuliko maslahi ya taifa. Ameeleza kuwa mara kadhaa ameomba chama chake kijiunge na UKAWA lakini CHADEMA wamekuwa wakigoma. Kauli ile ya jana sio ngeni masikioni pangu. Alieleza Zitto.

Zitto aliongezea kuwa, "kama ni matatizo basi ni kati yangu na viongozi wa CHADEMA na yasifanywe ya taifa zima. ACT-Wazalendo tuna nia ya dhati ya kuwaondoa CCM madarakani. Pia UKAWA wana nia hiyo hiyo. Kwa hali hiyo hatuna budi kushirikiana kummaliza CCM na hilo litafanyika kama kweli tumetanguliza utaifa mbele badala ya matatizo yetu binafsi na viongozi wa chama changu cha zamani."

My Take,

Zitto amekomaa kisiasa na ana ngozi ngumu sana. Pamoja na mihasira na Mbowe na maneno yake ya ovyo kuhusu Zitto, lakini kijana Zitto amemjibu kistaarabu sana na bado ameonyesha nia ya kutaka ushirikiano na UKAWA.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushakoroga zito umekuwa huaminiki wameghairi kukupenda.,yanini ulazimishe kutafuta kutetewa na wananchi??usitutie huruma pambana kivyako km ulivyoamua hukumuona Mrema na nccr na tlp alipiga kimyakimya na walimtambua hadi kesho yupo.,acha utoto kujitoa ufahamu wakati we mwnyw hujijui...usitafute pa kujificha ili utetewe huko ulipo ingilia mipango ya watu pia unaendelea kutibua,labda jiunganishe na ccm huku hatutaki watu wa aina yako,mchukua taarifa huku unapeleka kule,nimenukuu.,km huipendi potezea.......,

    ReplyDelete
  2. kweli zito mstaarabu hakika mungu yuko pamoja nae

    ReplyDelete
  3. aende ccm tu huyu, ni mlevi wa madaraka, labda ccm watampa cheo huko c mkombozi wakweli huyu

    ReplyDelete
  4. Kwanza atueleze huko alipo mambo yapo shwari???mi sielewi ndugu zangu kuhusu Act wazalendo wala Act Tanzania ni vyama viwili au ki1??maana ni ogopa sana kitu watu wameanzisha uje ulete mkanganyo hamuelewani ktk act labda nakuwa sielewi nini maana ya kiongozi na mwenyekiti dash!!!oya hii imekaaje wadau??kaka km kweli yanayosemwa kweli,sijui ulioewaga hela ili kuzima spidi yako nzuri ya utumishi,au hela ya kuhujumu chdm na bado nasoma habari unachonganisha unaona sasa hapo ndo patamu.,vp hapo ulipojishkiza maana Mungu akusaidie uwe salama sio kwako wenyewe wapo na wanakomaa na chama lao inaonekana hamjaenda sawa bora ungekubali kujishusha we unajiinua hawatakubali bila kufuata protoco zao.,yaaani nilitegemea baada ya chadema ungetulia kimya bila kutafuta ushindani wa kisiasa ili uonekane bado unaweza hpo ndo ulipokosea unaonekana mwaribifu ona chadema hamuelewani,act hsmjatulia bado tena na ukawa unataka??????khaaa aaaaasa haoana aisee ishia hapo au pumzika kidogo ndo dawa upende usipende ili watu tukumisi kidogo halafu ukirudi nguvu mpya.,sahivi unatumia nguvu nyingi Sana kupambana kuliko mwanzo wa harakati zako unajichosha kaka.,jipunguzie majukumu unaumia Sana,soma filipi 4:3 halafu Tulia ngoja wakati Wako bado unapumua nafasi unayo tchaooooo......,

    ReplyDelete
  5. ZITTO CHUMA CHADEMA MTAUWAWA NA MBATIA SUBIRI UTANAMNBIA

    ReplyDelete
  6. Chadema wanajua kuwa jamaa akiingia ukawa basi itakuwa purukushani katika kugawana majimbo, Jamaa hawezi buruzwa kama akina lipumba. Ila sasa ukawa wajue kuwa kila atakapowekwa mgombea wa ukawa lazima awagaragaze wengine. UZALENDO KWANZA UBINAFSI BAADAE

    ReplyDelete
  7. Zitto kiboko ya chadema mwaka huu watakoma paka mkongwe wao mbowe kaonyesha zahiri kua zitto atawakimbiza sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad