Nchi imeyumba, LOWASSA Ndiye wa Kuisimamisha na Kuirudisha Katika Mstari

Watanzania wenzangu ni wazi kuwa TANZANIA ya sasa inamhitaji kiongozi wa maamuzi na utendaji kama NGOYAYI, wazee mbali na serikali kusema kuwa watapata huduma za afya bure, ukweli ni huu, hakuna huduma hiyo ya bure wanayoipata zaidi ya kuteseka, na uthibitisho ni mzee aliyekuwa akiongea kwa uchungu siku ya kikao cha 4U movement pale LULUMA. Na alidiriki kusema wazi kuwa serikali hii ya JK imekosa mwelekeo, akimaanisha hakuna msimamizi wa sera wala mfuatiliaji.

Ndugu zangu, elimu ya sasa ya mfumo huu wa kuajiriwa ambayo haikidhi mahitaji ya ushindani katika dunia ya DIJITALI bado imeendelea kutopewa thamani wala kipaumbele, nayaongea haya kama mwezeshaji ama mdau katika sekta nadhifu ambayo ingesimamiwa kwa umakini Tanzania tusinge visikia vilio vya wananchi kuhusu ajira.
Elimu ingesaidia kutoa ajira kwa wahitimu kujiajiri wenyewe kwa kutumia maarifa na ujuzi waupatao mashuleni kuendeleza taifa lao. Elimu ndio chombo pekee ulimwenguni chenye uwezo wa kulikomboa na kuliendeleza taifa kama ikitumika kwa masilahi lengwa. Mimi kama mwalimu nimeipita sera ya Elimu iliyozinduliwa na Dkt. JK mwezi wa pili mwaka huu, katika kuisoma sera hiyo zaidi ilichojikita kuelezea ni mapungufu ya sera zilizopita kama sera ya mwaka 1999 na nyinginezo. Sera hii ya mwaka 2014 iliyozinduliwa mwaka huu hakika haitoi suruhisho la elimu ya Tanzania zaidi ya kujikita kulalamikia sera mbovu za nyuma.
Ukiona sera imekosa kuonesha namna ya kuisaidia elimu na ikajikita kuelezea matatizo ama mapungufu ya sera zilizopita ni wazi kuwa aliyeshindwa kusimamia hili si waziri mwenye dhamana bali hata aliyempa hiyo dhamana ya kusimamia elimu.

Itakumbukwa pia kuwa katika Bungr lililopita katika kujadili Mswada wa Sheria ya BARAZA LA VIJANA mama yetu Spika wa Bunge alikuwa akimtumia sana Tundu Mugwayi LISSU na Andrew CHENGE kuliko hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George MASAJU kwa kutambua uwezo wake kuwa mdogo. "Tundu Lissu, nadhani kipengele hiki mheshimiwa spika kingefaa kisomeke hivi" Anasimama Mwanasheria mkuu anapinga, mama Anna Makinda kwa kutoamini uwezo wa AG anaona amuulize Andrew Chenge, anaposimama Andrew Chenge anasema "Mheshimiwa Spika alivosema Tundu Lissu ni sawa"😳.

Imefikia hata viongozi wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani katika utendaji, Spika wa Bunge hamwamini AG, na AG ameteuliwa na Rais maana yake ni kwamba Spika wa Bunge hamwamini Rais, ndiyo tafsiri yake.
Ni lazima tushiriki kwa pamoja kumpata Rais mwenye uwezo wa kujua ya kwamba watanzania wanahitaji kama ni elimu basi iwe bora na yenye tija na kama ni viongozi wa kusimamia aidha Wizara au Vitengo ajue kuwa ni watu wenye uwezo kiutendaji na si mzigo hata kwa Viongozi wenzao. Spika hana imani na AG, je mtanzania wa kawaida atakuwa na imani nae?
LOWASSA namuona kuweza kuoongoza nchi hii,

Watanzania wamekata tamaa na Viongozi wao, na hata nchi yao pia, tumaini la maisha yao halipo tena, heshima ya nchi imepotea, Baba Rais, Mama Rais na hata Watoto ni Marais mfumo wa BMW, Baba, Mama na Watoto.

Nape Nnauye nakuomba uache kuwachagulia watanzania Rais, nchi hii si yako wala rafiki zako, bali ni ya watanzania wote na hao ndio wanamtaka NGOYAYI LOWASSA, wazee wa mkoa wa Singida wanakupa salamu wakisema Umwambie Mwenyekiti wa CCM kuwa akikosea kufanya maamuzi kwa masilahi yake na watu wake nchi hii isipokalika ajue ya ndiye chanzo na hawatakuwa tayari kuyavumilia haya, wataungana na watanzania wenzao kususia uchaguzi ili mtimize adhima yenu.

James LEMBELI anawaasa Viongozi wakubwa wa Chama Cha Mapinduzi kutofanya makosa ya kukata majina ya watu wanaokubalika na anasema wamkate yeye kama wanataka, huo ni ujumbe usiohitaji elimu kubwa kuelewa kuwa ameongea nini. CCM mlipoteza majimbo mengi ya uchaguzi mwaka 2010 kwa hira zenu binafsi kwa kuwaweka watu wasiokubalika na wananchi wa eneo husika, mfano ni Iringa mjini mlimuweka yule mama Mbega mkamkata Mwakalebela, Ubungo mkamuweka mama aliyelalamikia kuuza nyumba ya Urafiki na kumkata Nape aliyekuwa anakubalika kipindi hicho japo leo amekengeuka. Mimi ninaongea kama mtanzania ninayeipenda nchi yangu.

Maana nasikia sikia kuwa kuna wengine mmenunua mahekali huko nje ya nchi mkimaliza uongozi wenu mtaenda kuishi, nasema nasikia na sijamtaja mtu, ila mkae mkijua kuwa nchi hii isipokalika kwa kuweka mAsilahi yenu mbele hakika dhambi hiyo itawatafuna.

My take: Tuache viongozi wanaokubalika wawatumikie watanzania wenzao na si mnaowataka ninyi kwa masilahi yenu ya mfukoni.

Comrade mbobezi aliye amua kuifia nchi na watu wake,
George Sylvester Wambura (Prince George) via JF

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WERAWERA UMENENNA
    nO COMMENTIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad