PAUL MAKONDA Awa LULU Kinondoni, Wapinzani Wake Wabaki Midomo Wazi

Mtakumbuka kuwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais Jakaya Kikwete afanye uteuzi wa wakuu wa wilaya ambapo katika uteuzi huo, Paul Makonda Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa CCM akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wilaya yenye pilika na vurugu nyingi hapa Tanzania. Wengi walibeza uteuzi huo na wengine wakihoji uwezo wa Makonda mpaka kukabidhiwa wilaya kubwa ya Kinondoni. Viongozi wa vyama vya Upinzani hususan Henry Kilewo wa CHADEMA alianzisha mada humu kwa lengo la kumtisha Makonda kuwa anaingia kwenye wilaya ambayo itakuwa maji shingo kwake.

Kelele za wapinzani dhidi ya makonda zimetokana na jinsi alivyokuwa mahiri alipoteuliwa kuwa mbunge wa bunge maalum la Katiba. Hakika Makonda alionesha ukomavu mkubwa na alitoa michango yenye tija kwa taifa. Aidha, wengine walimbeza Makonda kutokana na msimamo wake wa kumpinga Edward Lowasa pale anapotumia fedha nyingi kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa. Sambamba na hilo, wengine wamemchukia Makonda kwa kuweka bayana msimamo wake wa kutokubaliana na midahalo iliyokuwa inaandaliwa na iliyokuwa tume ya mabadiliko ya Katiba chini ya Joseph Warioba. Tena ilifika wakati Paul Makonda alisingiziwa kuwa amempiga Warioba ilhali ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemnusuru kipigo kutoka kwa wahuni wa CHADEMA ambao waliandaliwa kuvuruga mdahalo huo ili ionekane kuwa ni CCM ndio waliovuruga.

Akiwa amekaa madarakani chini ya miezi miwili tu, Makonda ameonesha kuwa ni mchapa kazi na jasiri mkubwa katika kushughulikia kero zinazowakabili wana Kinondoni. Makonda ameonekana kuwa ni mfanya maamuzi sahihi. Mathalan, ameamua kuwa katika hospitali za Manispaa ya Kinondoni hasa Mwananyamala, Kuwe na Dawati la Polisi ambalo watashughulikia huduma za PF 3 ambazo kabla ya hapo, majeruhi walikuwa wanatakiwa kwenda kwanza kituo cha polisi kupata huduma hiyo kabla ya kwenda hospitali.

Aidha, Hivi karibuni, Paul Makonda ameunda Kamati kushughulikia ujenzi mbovu wa barabara za manispaa ya Kinondoni. Mtakumbuka kuwa Kinondoni inaongoza kwa kuwa na barabara za lami zinazojengwa na kuharibika ndani ya muda mfupi. Barabara za kutoka Kinondoni Biafra hadi Bestbite Namanga, barabara ya Hubert Kairuki na barabara ya Mwanyamala Hospitali ni mfano wa barabara ambazo zimejengwa na kuharibika ndani ya miezi sita tu tangu kukamilika ujenzi.

Kwa haya machache, hata akina Hemry Kilewo ambao walimshambulia kabla hajaaapishwa, leo wamebaki midomo wazi na wamebaki kumshangilia na kumpigia makofu. Hata humu jf, zile mada zilizokuwa zinaanzishwa na BAVICHA za kumshambulia Makonda zimepungua. Hakika Makonda umeonesha mfano mzuri kwa vijana wa hapa nchini. Endelea kuwajibika kwani wana Kinondoni wana imani na wewe.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna lolote!! tunajua wewe ni mpiga debe wake hana jipya mpaka sasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad