Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo
Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa
Huyu ndio muwekezaji wa kweli
ReplyDeleteHII NI KOMESHA NA KALI ZAIDI, NCHI NDANI YA NCHI- "BiLionea Alhaji Aliko Dangote amekabidhiwa hekari 2,500, katika halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi"
ReplyDeleteWaswahili walisema HABA NA HABA HUJAZA KIBABA"iuzeni tu nchi ya bongo tuje tutawaliwe tena kama b4 za enzi zilie za waingereza na wajerumani UKOLONI MAMBO LEO"mnaiuza nchi hata hampigi picha ya kuwa in future coming years itakuwaje na mtanzania atakuwa katika hali gani?Kuuza nchi kutamsaidia mtanzania au?Kweli you've to live and learn
ReplyDeleteNajua angepewa mzungu ungeridhia ila mwafrika hutaki,hovyo!
Deletehiyo ni sawa na sahihi kabisa kwa sababu nchi yenyewe iliisahau mtwara......na kingine sioni ubaya kuwapa waafrika wenzetu ardhi kwani tunapoelekea tunataka baadae afrika yetu iwe moja so hivyo ni moja ya vitu vinavyoimarisha ushirikiano kati yetu na si kuwapa wazungu ambao lengo langu ni kutunyonya tu........bt lakini mi nadhani hata madini tungempa huyu jamaa na si wazungu
ReplyDeleteHehehehehhehehe hiyo kali.... haya bwana watu na pesa zao....
ReplyDeleteKweli kabisa apewe na madini
ReplyDelete