Watu 10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.
Akizungumza na Mwandishi wetu Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda, gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.
Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
Ukiona magari yanagongana uso kwa uso ujue madeleva si wazoefu
ReplyDeleteMadereva acheni mchezo wenu mbaya wa kuwapa makondakta kuendesha wakati mkiwa na abiria kumbukeni nyie siyo waalimu wa kufundisha kuendesha kuna shule maalum za kujifunza kuendesha (driving schools ) nimesafiri mara nyingi nimeona huu mchezo ukifanyika ghafla konda naye anashika usukani. Fuateni sheria za kuendesha overtaking zisiso za mhimu ziacheni.so sad
ReplyDelete